Home Michezo TANZIA:MCHEZAJI WA MTIBWA SUGAR,AZAM FC NA CHUONI FC AFARIKI DUNIA

TANZIA:MCHEZAJI WA MTIBWA SUGAR,AZAM FC NA CHUONI FC AFARIKI DUNIA

0

IBRAHIM Rajab maarufu kwa jina la Jeba, ambaye alikuwa kiungo wa zamani wa timu ya  Mtibwa Sugar yenye maskani yake Morogoro na Azam FC ametangulia mbele za haki.

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo alikuwa akipatiwa matibabu katika  Hospital ya Mnazi Mmoja, visiwani Zanzibar.

Jeba kabla ya umauti wake alikuwa anaitumikia timu ya Chuoni FC ya Visiwani Zanzibar.