Home Mchanganyiko TBL yaadhimisha Siku ya Uhamasishaji Unywaji Bia Kistaarabu Duniani kwa vitendo

TBL yaadhimisha Siku ya Uhamasishaji Unywaji Bia Kistaarabu Duniani kwa vitendo

0

Wafanyakazi wa Comfort hotel Mbeya wakifuatilia mafunzo

Wafanyakazi wa TBL Arusha wakionyesha mabango ya uhamasishaji.

Wafanyakazi wa baa ya Kwetu Pazuri wakifuatilia mafunzo.

Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakionyesha mabango ya uhamasishaji wakati wa maadhimisho hayo.

Afisa Masoko wa TBL kiwanda cha Mwanza , Happy Conrad, akitoa elimu ya kunywa kistaarabu kwa wahudumu wa baa ya Las Vegas, iliyopo Bwiru jijini Mwanza.

Meneja Masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi,akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa baa ya Tips iliyopo Mikocheni Dar es Salaam.

******************************

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) mwishoni mwa wiki ilifanya maadhimisho ya Siku ya Bia Duniani 2019, (Global Beer Responsible Day), ambapo wafanyakazi wake kutoka viwanda vya Dar Es Salaam,Mwanza, Mbeya na Arusha, walishiriki kufanya uhamasishaji wa unywaji wa bia kistaarabu kwa wateja na wafanyakazi katika mabaa mbalimbali.

Kauli mbiu ya  maadhimisho hayo ambayo wateja wake wengi wameyafurahia ni  100% Jiachie .100% Kwa kiasi. # Jipimie!)