Home Mchanganyiko SOKO LA MIFUGO NA MAZAO YA MIFUGO LIMEPATA MATUMAINI MAPYA YA KUFANYA...

SOKO LA MIFUGO NA MAZAO YA MIFUGO LIMEPATA MATUMAINI MAPYA YA KUFANYA VIZURI

0
 ,Meneja wa Wakala wa Maabara za Vetinari(TVLA)mkoani Tanga Dkt. Imna Malele akizungumza katika mafunzo ya siku mbili ya uandishi wa habari za kisayansi kati ya watafiti na waandishi wa habari wa mikoa ya Tanga, Pwani na Morogoro yaliyofanyika jijini Tanga yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania(TALIRI) kwenye ofisi za Kanda inajumuisha mikoa ya Dar,Pwani Morogoro na Tanga Dkt. Zabron Nziku wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za sayansi na teknolojia yanayofanyika mjini Tanga.

Afisa Utafiti Mkuu kiongozi kutoka Tume ya Sayansi na teknolojia Dkt Bakari Msangi akitoa mada kwenye mafanzo hayo kuhusu umuhimu wa utafiti nchini Tanzania pamoja na umuhimu wa kusambaza matokeo ya utafiti

 KAIMU Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarufa Costech Emanuel Abiner kushoto akiwa na akiwa na Dkt Janet Kaaya ambaye ni Science Communications Specialist wakiwa kwenye mafunzo hayo
 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania(TALIRI) kwenye ofisi za Kanda inajumuisha mikoa ya Dar,Pwani Morogoro na Tanga Dkt. Zabron Nziku  akiwa na washiriki wengine kwenye mafunzo hayo
 Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo hayo
SOKO la mifugo na mazao ya mifugo mkoani Tanga limepata matumaini mapya ya kufanya vizuri baada ya Taasisi ya Chanjo ya Mifugo Tanzania (TVI) iliyopo Kibaha mkoani Pwani kugundua aina tano za chanjo za mifugo.
Chanjo hizo ni CBPP ya homa ya mapafu ya ng’ombe, S-19 Brucellosis kwa ajili ya ugonjwa wa ng’ombe kutupa mimba, chanjo ya ugonjwa wa kimeta(anthrax),ugonjwa wa ng’ombe wa chambavu (BQ)  na ya ugonjwa wa kideri cha kuku.
Chanjo hizo za magonjwa ambayo yamekuwa yakiwasumbua mara kwa mara mifugo aina ya ng’ombe na kuku na kusababisa vifo si kuleta hasara kwa wafugaji,pia kupoteza ubora wa mazao ya mifugo.
 Akizungumza katika mafunzo ya siku mbili ya uandishi wa habari za kisayansi kati ya watafiti na waandishi wa habari wa mikoa ya Tanga, Pwani na Morogoro yaliyofanyika jijini Tanga yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ,Meneja wa Wakala wa Maabara za Vetinari(TVLA)mkoani Tanga Dkt. Imna Malele amesema mkoani Tanga chanjo hizo zimeleta matumaini mapya kwa wafugaji.
Amesema kuwa awali wafugaji wengi walikuwa wanapata hasara na mifugo mingi kuteketea kutokana chanjo hizo nyingi zilikuwa zinaagizwa kutoka nje ya nchi zilikuwa ghali.
Amefafanua kuwa mkoani Tanga haswa maeneo ya wafugaji katika wilaya za Handeni, Kilindi, Pangani,Tanga Jiji,Lushoto na Mkinga ng’ombe walikuwa wanasumbuliwa na magonjwa ya homa za mapafu, chambavu, kimeta na ugonjwa wa kutupa mimba. “Ugunduzi wa chanjo hizi umeleta ufumbuzi kwa wafugaji mkoani Tanga haswa kwenye maeneo yenye wafugaji wengi kutokana na chanzo hizi kuwa mkombozi kutokana na bei yake na zianendana sambamba na mifumo ya ng’ombe kutokana zilizotengenezwa “alisema.

 Ameongeza “kutokana na ubora na gharama yake kuwa chini wafugaji wengi wamekuwa wakizikimbilia”.
 Katika hatua nyingine Dkt. Malele amesema kuwa Wakala wa Maabara za Vetinari (TVLA) nchini kwa kushirikiana na na Taasisi  ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo ya Kenya (KALRO) wamegundua kemikali zenye harufu ya mnyama aina ya kuro ambaye harufu yake inafukuza wadudu wasumbufu kwa ng’ombe aina ya Mbung’o.  
Amesema kuwa harufu hiyo watawekewa ng’ombe kwenye kifaa maalum watakachofungwa nacho sikioni ili akijitikisa inamsaidia kusambaza harufu hiyo ya kemikali ambayo inafukuza Mbung’o na sasa wapo katika hatua za kusajili

Mfugaji Mwekezaji wa Kijiji cha Zeneth anayejishughulisha na Kilimo na Mifugo Robert Johnson ambaye ana shamba la mifugo ya kuku,ng’ombe wa maziwa na nyama amesema kuwa  mifugo yake ilikuwa inapata maradhi na alikuwa anaagiza chanjo na dawa za mifugo kutoka nje nchi Uholanzi na Denmark lakini baada ya TVI kufanya ugunduzi huo amepata nafuu na suluhisho kutokana amepunguza idadi ya vifo vya wanyama na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo kutokana na chanjo hizo kupatikana kwa urahisi.