Home Mchanganyiko BENKI YA KCB YAENDELEA KUSIMAMA NA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI (SME) 

BENKI YA KCB YAENDELEA KUSIMAMA NA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI (SME) 

0

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya KCB Christina Manyenye, (kulia), akizungumza na wafanyabiashara zaidi 300 wakati wa kongamano la KCB Biashara Club liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kutoa mafunzo katika nyanja mbali mbali za kuendesha biashara, fursa ndani ya Biashara Club na utayari wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wateja wake wanachukua  fursa hizo.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya KCB, Nd. Masika Mukule akijibu swali kutoka kwa mmoja ya wafanyabiashara zaidi 300 wakati wa kongamano la KCB Biashara Club liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kutoa mafunzo katika nyanja mbali mbali za kuendesha biashara, fursa ndani ya Biashara Club na utayari wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wateja wake wanachukua  fursa hizo.

Mkuu wa Kitengo Wafanyabishara Wadogo na wa Kati (SME) wa Benki ya KCB, Abdul Juma (kulia), akizungumza na wafanyabiashara zaidi 300 wakati wa kongamano la KCB Biashara Club liliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kutoa mafunzo katika nyanja mbali mbali za kuendesha biashara, fursa ndani ya Biashara Club na utayari wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wateja wake wanachukua  fursa hizo.

………………..

Benki ya KCB Tanzania yaendelea kusimama na wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kuandaa kongamano la pili la KCB Biashara Club. Kongamano hilo lilifanyika jijini Serena Hotel jijini Dar es Salaam na kuleta pamoja wafanyabiashara zaidi ya 300. Programu KCB Biashara Club ilibuniwa na benki hiyo kwa dhumuni la kutoa fursa mbali mbali kwa wafanyabiashara zikiwemo mafunzo ya uendeshaji biashara, kuwapa wafanyabiashara jukwaa la kushirikiana pamoja na kuwakuzia mtandano wa masoko ndani na nje ya Tanzania. 

Tangu kuanzishwa kwake, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara. Mwezi Machi Mwaka 2019, Benki ya KCB iliendesha kongamano kama hili jijini Arusha hususan kwa wafanyabiashara walio katika sekta ya utalii. 

Akiongea wakati wa kufungua semina hiyo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bi. Christine Manyenye alisema Benki ya KCB imefanya juhudi za mahususi za kuwaleta wadau kama Injinia Jane Kadoda kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambaye aligusia athari za biashara kwa mazingira pamoja umuhimu wa kutii sheria za kulinda mazingira zilizowekwa na serikali ya Tanzania. Kwa upande wake mdau kutoka European Investment Bank (EIB), Nd. Fasili Boniface aliongelea umuhiumu wa kuweka kumbukumbuku za kifedha na jinsi ya kuainisha matumizi ya binafsi na ya kibiashara. 

Bi. Saada Sipemba kutoka Sadio Travel and Tourism ambaye ni mtaalamu wa safari za kibiashara aliongelea fursa za kibiashara zinazopatikana nchini China na juhudi za benki hiyo kuhakikisha inawatengenezea wateja wake mianya ya kuchukua fursa hizo kwa urahisi. Benki ya KCB Tanzania kupitia Biashara Club imekuwa ikiandalia wadau wake safari za kibiashara kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini kwa gharama nafuu kwa dhumuni la kuwafungulia masoko mapya na bidhaa nafuu za kuleta kwenye soko la Tanzania. 

Mbali na kufaidika na ujuzi wa kupitia semina na safari mbalimbali zinazoandaliwa na KCB Biashara Club, wanachama pia wanafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao unaopelekea kuongeza ujuzi na kupanua wigo wa biashara. KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara wadogo na wa kati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara. 

Kuhusu Benki ya KCB 

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki. 

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro. 

Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.