Home Mchanganyiko IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA UKAGUZI ZANZIBAR NA KUKAGUA MIRADI YA UJENZI...

IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA UKAGUZI ZANZIBAR NA KUKAGUA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA ZA ASKARI

0

******************************

10/09/2019 ZANZIBAR

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema hali ya usalama katika
visiwa vya Zanzibar imezidi kuimarika kutokana na ushirikiano uliopo kati ya
Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi wa visiwani humo.

IGP Sirro ameyasema hayo leo wakati akiwa katika ziara ya siku moja visiwani
humo ambapo amekagua miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari
pamoja na kutembelea eneo la uwanja wa mbinu za medani lililopo Kiashange,
Kaskazini unguja.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Utawala Zanzibara Naibu Kaimishna wa Polisi
DCP Faustine Shilogile amesema kuwa, ujenzi wa nyumba za Polisi visiwani
humo utasaidia katika kuimarisha suala la uwepo wa makazi bora ya askari na
familia zao.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCP
Ahmed Msangi amesema kuwa, jeshi la Polisi kwa upande wa Zanzibar
limejipanga katika kuhakikisha kuwa linawachukulia hatua kali za kisheria watu
wanaojihusisha na uingizaji na usafirishaji wa dawa za kulevya na kwamba hadi
kufikia sasa watu kadhaa wamekamatwa kutokana na kujihusisha na vitendo
hivyo.