Home Mchanganyiko MAHAKAMA INAYOTEMBEA DAR YAENDELEA NA KAZI

MAHAKAMA INAYOTEMBEA DAR YAENDELEA NA KAZI

0

Mwananchi, Zubeda Abdallah Kombo akielekezwa na Karani wa Mahakama ya Mwanzo, Kimara,Judith Mwakyalabwe jinsi ya kupata hati ya kiapo.

Karani wa Mahakama ya Mwanzo, Kimara, Judith Mwakyalabwe, akiendelea na utendaji kazi ndani ya Mahakama Inayotembea wakati Mahakama hiyo ikitoa huduma eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, iliyopo Kibamba jijini Dar es Salaam.

Gari ya Mahakama Inayotembea likiwa katika eneo ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo, iliyopo Kibamba jijini Dar es Salaam likiendelea kutoa huduma za kimahakama.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ya Kimara, Mhe. Geiza Mbeyu, akimsikiliza kwa makini mwananchi ambaye alikuwa akiuliza jambo kuhusu Mahakama Inayotembea katika eneo la Stendi ya Kibamba iliyopo jijini Dar es Salaam.

Picha na Aziza Muhali (SJMC)