Home Mchanganyiko TETEMEKO LA ARDHI LAZUA TAHARUKI KWA WAKAZI WA KATAVI

TETEMEKO LA ARDHI LAZUA TAHARUKI KWA WAKAZI WA KATAVI

0

Baadhi ya nyufa zilizojitokeza katika nyumba baada ya tetemeko

********************

Na Mwandishi wetu, Katavi

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 5.5 lililotokea usiku wa kuamkia leo mkoani Katavi limezua taharuki kubwa kwa wananchi

Tetemeko hilo lililotokea majira ya saa tisa usiku limesababisha baadhi ya watu kulala nje kwa kuhofia kuangukiwa na nyumba zao huku kuta za nyumba kadhaa zikiachwa na nyufa

Aidha tetemeko hilo lilipiga tena majira ya saa 12 na saa mbili asubuhi

Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa tukio hilo lilikuwa la kuogofya hali iliyopelekea kukimbilia nje na familia zao

Komredi Juma Homera ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi amesema hakuna madhara ya kibinadamu yaliyojitokeza kufuatia tetemeko hilo

Ameongeza kuwa baadhi ya nyumba zimepata nyufa lakini hakuna taarifa ya mtu yeyote kupoteza maisha ama kujeruhiwa

Aidha ameiomba mamlaka ya hali ya hewa kuangalia uwezekano wa kutoa taarifa mapema ili kuepusha majanga

“Wananchi wengi hawajui namna ya kujilinda na tetemeko kwahiyo linapotokea inakuwa ni taharuki kubwa” alisema Homera