Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza katika Kongamano la Tisa la wajane lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha St. John jijini Dodoma.
Baadhi ya wajane wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano la Tisa la wajane lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha St. John jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akisalimiana na baadhi ya wajane mara baada ya kufungua Kongamano la Tisa la wajane lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha St. John jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiwa katika picha ya pamoja na mara baada ya kufungua Kongamano la Tisa la wajane lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha St. John jijini Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
……………………
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa mila na Dini zisizo na hitilafu haziwezi kuruhusu wajane kunyanyaswa katika jamii.
Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Tisa la wajane lilioandaliwa na Taasisi ya ‘Amazing Grace’ kwa lengo la kuwajengea uwezo wajane ili waweze kupambana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika jamii
Dkt. Jingu ameongeza kuwa jamii inawajibu wa kumlinda mjane na vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi yake kwani hata vitabu vya dini vimeipa jamii jukumu hilo la kuwasaidia na kuwalinda wajane dhidi ya unyanyasaji wowote katika jamii.
Aidha Dk. Jingu amesema kuwa hakuna mila wala dini zilizo nzuri zinazoruhusu wajane kunyanyaswa, kunyanganywa nyumba zao na kudhulumiwa haki zao za msingi kama ardhi, nyumba, magari na mali nyinginezo na hata wakati mwingine kunyanganywa watoto.
Aidha Dkt. Jingu amesema kuwa wajane ni kundi maalum katika jamii ambalo Serikali, jamii na mtu mmoja mmoja tuma wajibu wa kuwalinda na hivyo Serikali imejidhatiti katika kuwasidia wajane kutatua changamoto zao.
Ameyataja mambo hayo kuwa ni utoaji wa elimu bure ambapo watoto wengi ambao ni yatima kutoka familia za wajane wameweza kupata fursa ya elimu ya msingi, sekondari na hata kufikia vyuo vikuu, uwepo wa mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inayosaidia kuwapa wajane mikopo inayowawezesha kujikwamua kiuchumi.
“Hakuna mila wa Dini inayoruhusu wajane wanyanyaswe ila kama zipo basi zitakuwa na hitilafu na hazifai katika jamii” alisema Dkt. Jingu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya “Amazing Grace” Bw. Paulo Mwanga ametoa wito kwa jamii kuacha kuwafanyia wajane vitendo vya kikatili vya uonevu ili wajane hao waweze kuishi kwani mama mjane akipoteza amani jamii nzima inakosa amani na tutakuwa na familia legelege kiuchumi, kijamii, na kiutamaduni maana wajane ni sehemu ya jamii ambayo ni nguvu kazi ya jamii na wanatakiwa kutendewa haki ili kujenga Taifa imara.
Naye mmoja wa mjane Bibi. Beatrice Muinuka kutoka mkoa wa Mbeya amesema kuwa kongamano hilo limewasaidia kutambua haki zao kama wajane na wanaishukuru Serikali kwa hatua mbalimbali ikiwemo fursa mbalimbali katika maeneo yao ya kuweza kupata mikopo itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi na kuendesha maisha yao.
Shirika la “Amazing Grace” limeandaa Kongamano la wajane la wiki moja jijini Dodoma linalolenga kuwajengea uwezo wajane kiroho na kimwili ikiwemo kupata mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kujikwamua kiuchumi, Kongamano hilo limeshirikisha Wajane kutoka ya Congo, Malawi, Kenya na Tanzania.