Home Michezo WAKAZI WA KATAVI WAMESHIRIKI MBIO ZA RIADHA KUCHANGIA HOSPITALI

WAKAZI WA KATAVI WAMESHIRIKI MBIO ZA RIADHA KUCHANGIA HOSPITALI

0

Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera akizungumza na wananchi katika uwanja wa Azimio

Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera akiwa na viongozi wengine wakipasha misuli kabla ya mbio kuanza.

Mshindi namba moja wa mbio kilometa 20 Fillingson Singyi akiwa amekamilisha mbio hizo.

**************

Na Mwandishi wetu,  Katavi 

Wakazi wa mkoa wa Katavi kwa mara ya kwanza wamejitokeza kushiriki mchezo wa mbio za riadha za kilometa 20, kilometa 10, 5, 3 na 1 zinazojulikana kwa jina la Homera Marathon kwa lengo la kuchangia fedha za ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi inayokabiliwa na uchakavu mkubwa

 

Mbio hizo zimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ambaye amewataka wakazi wa mkoa huo kuchangia hospitali hiyo

 

“Tuna namba za simu na akaunti za benki ambazo kila mwananchi anaruhusiwa kuchangia” alisema Homera

 

Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wameeleza dhana nzima ya mbio hizo kuwa ni pamoja na kuimarisha afya pia itaboresha miundombinu ya hospitali hiyo

 

Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo sasa inatumika kama Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ilijengwa tangu mwaka 1952 inakabiliwa na uchakavu mkubwa