Home Mchanganyiko MWILI WA BAROZI KADUMA WAZIKWA NJOMBE

MWILI WA BAROZI KADUMA WAZIKWA NJOMBE

0
NJOMBE

Mwili wa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje katika serikali ya awamu ya kwanza Ibrahim Kaduma aliyefariki dunia wiki iliyopita nchini India na kurejeshwa nchini umefanyiwa ibada maalumu katika kanisa la kuu la kiinjili la Kilutheli Tanzania mkoani Njombe na kupumzishwa katika makazi ya milele Nyumbani kwake katika mtaa wa Kibena Mjini Njombe.

Kaduma amelizaliwa 1937 na kufariki dunia 2019 akiwa na miaka 82.

Zoezi la kuombea mwili na mazishi ya mwanasiasa huyo mkongwe ambaye alifanya kazi kwa karibu na makanisa mbalimbali nchini limeongozwa na askofu mkuu wa KKKT Tanzania Dr Fredrick Shoo ambapo katika ibada hiyo maalumu askofu huyo amesema taifa na kanisa limepoteza mtu muhimu ambaye alikuwa akihimiza suala la maadili ya taifa na imani katika muda wake wote.

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka akitoa salamu za serikali huku akiwa ameambatana na makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi bara Philipo Mangula amesema mzee kaduma ni miongoni mwa waasisi wa taifa ambao wamehudu kwa weledi na uzalendo mkubwa kwa muongozo wa misingi ya maadili ya utumishi wa umma.

Kwa upande wao baadhi ya waombolezaji kutoka taasisi na mataifa mbalimbali akiwemo Christopher Mwakasege wamepata wasaha wakumuelezea marehemu enzi za uhai wake.

Mbali na kuhudumu katika nafasi ya waziri wa mambo ya Nje, Kaduma pia enzi za utumishi wake amekuwa barozi,waziri wa biashara ,waziri wa mawasiliano na nafasi nyingine za juu.