Pipipiki za matari matatu  maarufu kama bajaji zilizokuwa zimefunga barabara ya Mjini – Masika  Manispaa ya Morogoro.

 Pipipiki ya matari matatu  maarufu kama bajaji ikipandishwa kwenye gari la manispaa baada ya kukamatwa katika operesheni  ya kuziondoa pikipiki hizo zilizokuwa zimefunga barabra.

Baadhi ya Madereva wa  Pipipiki ya matari matatu  maarufu kama bajaji wakiwa katika mgomo.

……………………………………………………

NA FARIDA SAIDY, MOROGORO

MADEREVA wa  Pipipiki ya matari matatu  maarufu kama bajaji ambao wanatoa huduma ya usafiri  manispaa ya Morogoro wamefunga barabara ya Mjini – Masika  kwa saa kadhaa wakishinikiza uongozi wa mansipaa ya Morogoro na kikosi cha usalama barabarani  kuwaaacha waendele na zoezi la kupaki pikipiki hizo katika eneo la Islamu na Luna hali iliyolizazimu jeshi la polisi kuingilia kati na kuwaondoa kwa nguvu .

Akizungumza mara baada ya operasion hiyo mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Michael Deleli amesema kuwa  wamelazimika kuwaondoa ili kupunguza msongamano wa watu katika barabara hiyo ambao ulikuwa unasababaishwa na  kuengesha bajaji bila ya utaratibu kama anavyoleza

Mhandisi Godwini Mpinzile  ni mratibu Wakala wa barabara vijiji na mjini TARURA amesema  madereva hao walishapewa maelekezo sehemu za kwenda kuegesha     bajajai zao lakini wamekuwa wakikaidi kufuata malelekezo hayo huku afisa mfawidhi mamlaka ya Uthibiti wa usafiri  wa ardhini LATRA Bw. Adrew Mlacha  ametolea ufafanuzi suala la leseni za  bajiji na utaratibu wa kufuata wakati wa kutoa huduma ya usafiri.

Nao baadhi ya madereva wa bajaji  akiwemo Bw. mfaume Yasini na Bw. Daudi Zungu  wamesema hawakati kuondoka katika eneo hilo lakini wameomba kuboreshewa mazingira kama madereva wa  magari kwani nao wanalipa ushuhuru kama vyombo vingine vya usafiri.

Hayo Yamejiri Baada Ya Halamshauri Ya Manispaa Ya Morogoro Kutoa Maelekezo Kwa Waendesha Babaji Kurejea Katika Vituo Vilivyopangwa Kuanzia Tarehe 5 Mwezi 9 Mwaka 2019.