Home Mchanganyiko Mwenge wa Uhuru wazindua Kituo cha Uzalishaji Umeme Jua

Mwenge wa Uhuru wazindua Kituo cha Uzalishaji Umeme Jua

0

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ali akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha  Power Corner katika kijiji cha m, Mgambo wilayani Sikonge.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa kituo cha uzalishaji wa umeme wa jua wa Power Corner katika kijiji Mgambo wilyani Sikonge mkoani Tabora.

Meneja wa Mauzo Kanda ya Magharibi Erick Francis akizungumza na waandishi wa habar mara baada ya mwenge wa uhuru kuzindua mradi wa kituo cha uzalishaji umeme jua katika kijiji cha Mgambo wilayani Sikonge mkoani Tabora.

kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ali akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kituo cha uzalishaji wa umeme jua katika kijiji cha Mgambo wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

watendaji wa kampuni ya power corner wakiwa katika kibao cha uzinduzi wa kituo cha uzalishaji umeme jua mara baada ya kuzindua kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mkongea Ali katika kijiji cha Mgambo wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Mhandisi Umeme wa Kampuni ya Power Corner Deogratias Hyera akimpa maelezo .Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ali kuhusiana na mtambo wa kuzalisha umeme jua katika kijiji mgambo wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

*****************

Na Chalila Kibuda
WANANCHI wa Kijiji cha Mgambo kilichopo Kata kitunda Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora wamesema kuwa kupata umeme kumeongeza fursa ya ajira katika kijiji hicho.
 
Umeme huo  umetekelezwa na kampuni ya Power Corner uliogharimu zaidi ya bilioni moja na kuunganisha kaya 195.
 
Wamesema kuwa hivi sasa kijiji cha kitunda kinafurahia huduma hiyo ya umeme jua na kwakweli umewezesha vijana kuweza kujiali kwa kujishughuli na mambo mbalimbali ya uzalishaji.
 
Hayo aliyasema  kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Ali wakati wa kuzindua  mradi wa umeme jua unao zalishwa na kampuni ya power corner.
 
Akizungumza kwaniaba ya Wananchi wezake Mzungu Maji ya Soda, alisema wanaipongeza sana Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Power Corner ambao ndio watekelezaji wa mradi kwani hivi wanakunywa maji baridi,nyama safi ambazo zinahifadhiwa kwenye friji,ukikinganisha na awali.
 
Pia alisema mradi huo wameupokea kwa mikono miwili na kwakweli hawakutegemea kulingana na historia yake kwani awali walikuwa wanatumia umeme wa sola ya kawaida za kufunga wenyewe ambao pia ulikuwa hauna nguvu kama ulivyo huo uliozinduliwa mwenge wa Uhuru.
 
“Nataka niwaeleze ndugu waandishi wa Habari leo vijana wetu wanatengeneza Simu hapahapa pindi zinapoharibika,wachomeleaji wamerahisishiwa,saluni zinafunguliwa kwakweli mambo mazuri sana.” Alisema Anthon Lukas.
 
Lukasi aliongeza kuwa ujio wa Umeme umeongeza chachu kwa wananchi kuweza kufanya kazi lakini pia umeimarisha usalama katika makazi ya watu ukilinganisha na huko nyuma.
 
  Naye mkazi mwingine John Bernard Fundi Simu alisema awali walikuwa wanalazimika kwenda Sikonge kutengeneza lakini hivi sasa kwakweli wanafurahia ujio wa Umeme jua huo.
 
Naye Meneja Mradi Kanda ya Magharibi Kutoka Kampuni hiyo ya Power Corner  Erick Francis akizungumzia mradi huo alisema Kampuni imepata ushirikiano mkubwa Kutoka mamlaka za Serikali katika kung’amua vijiji stahiki vya kupata huduma ya umeme.
 
Alisema kuwa mradi huo uliazishwa rasmi mwanzoni mwa mwezi machi 2018 ambao unauwezo wa kuzalisha kilo-whatts 20 kwa kijiji cha Mgambo na umeme wenye uwezo kilo-whatts 28kwa vijini vya mkola na Mwenge.
 
Kwaupande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Mzee Ali  akizungumzia  mradi ,kwanza alipongeza Serikali kwa kuweka Mazingira wezeshi kwa Kampuni ya Power Corner na kufikia hatua ya kuwapatia umeme wananchi.
 
“Nawaomba ndugu zangu  wa Kijiji hiki cha  Mgambo muweze kuulinda mradi huu ambao naamini umeleta fursa kubwa kwenu katika kuongeza uzalishaji Mali na kujiongezea kipato.” Alisema Ali.
 
Alisema kuwa mradi ni mzuri na kwakuwa ameridhishwa na kiwaKanda ha ujenzi wake na Fedha ilitotumika hivyo ameuzindua rasim kupitia Mwenge wa Uhuru.