Home Mchanganyiko MBULU WAMFAGILIA MAGUFULI

MBULU WAMFAGILIA MAGUFULI

0
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Joseph Mandoo akifungua kikao cha Baraza la madiwani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
……………….
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara limempongeza Rais John Magufuli kwa kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali ya wilaya na jengo jipya la utawala la makao makuu ya halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Joseph Guulo Mandoo alisema wanampongeza Rais Magufuli kutokana na kufanikisha miradi hiyo ya maendeleo.
Mandoo alisema hivi sasa halmashauri ya Mbulu imepiga hatua ya maendeleo kwenye sekta ya elimu, afya, utawala, miundombinu na maendeleo mengine.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Hudson Starnley Kamoga alisema kutokana na kutengwa kwa fedha hizo na Rais Magufuli, hivi sasa wanazidi kupiga hatua ya maendeleo kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Jengo la utawala la makao makuu linaendelea vizuri na hospitali nayo inaendele kujengwa kule kata ya Dongobesh, natarajia tutamaliza kipindi cha miaka mitano tukiwa tumehamia Dongobesh,” alisema Mofuga.
Alisema wanatarajia kutenga eneo la kumbukumbu la kuandika majina yote ya madiwani waliokuwepo madarakani waliopo madarakani wakiongozwa na Mwenyekiti Mandoo na mkurugenzi Kamoga.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga alisema Rais Magufuli amefanya maendeleo mengi ikiwemo miradi ya kimkakati kwa muda mfupi wa miaka minne aliyoongoza, utadhani amekaa madarakani miaka 40.
“Tumeona barabara za gorofa, elimu bila malipo, reli ya kisasa, umeme, hospitali mpya za wilaya zimejengwa vituo vya afya, utadhani ameongoza kwa miaka 40 kumbe ni miaka minne,” alisema Mofuga.