Home Mchanganyiko KAMANDA MUTAFUNGWA – MARUFUKU KUUZA PETROLI NA DISIEL PEMBEZONI MWA BARABARA BILA...

KAMANDA MUTAFUNGWA – MARUFUKU KUUZA PETROLI NA DISIEL PEMBEZONI MWA BARABARA BILA YA LESENI,MOROGORO

0

***********

NA FARIDA SAIDY,MOROGORO

JESHI la polisi mkoani Morogoro limewataka wananchi wanaofanya
biashara ya kuuza mafuta ya Petroli na dizeli kiholela pembezoni mwa
barabara bila ya kuwa na leseni ya kufanyia bishara hiyo kuacha kufanya
hivyo mara moja.

Ili kupunguza matukio ya wizi mafuta katika magari ya mizigo hasa
nyakati za usiku sambamba na kuondokana madhara mengine ya kiafya
yanayoweza kujitokeza kutokana na kukaa na mafuta hayo majumbani.

Rai hiyo imetolewa na kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro (SACP
)Wilbrod Mutafungwa wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya
Dumila wilayani Kilosa ambapo amesema kuwa kumekuwa na tabia ya
baadhi ya watu kufanya bishara hiyo za kuuza mafuta pembeoni mwa
barabara jambo ambalo linahatarisha maisha yao kwani wengi wao
huchanganya mafuta pamoja na chakula ,bila kujali
madhara yatakayotokea.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano
huo wamelishukuru jeshi la polisi kwa kutoa elimu mbalimbali juu ya
udhibiti wa matukio ya vitendo vya kiharifuu