Home Mchanganyiko KAMATI ZA CHAMA CHA WABUNGE CPA KANDA YA AFRIKA ZAKUTANA MJINI ...

KAMATI ZA CHAMA CHA WABUNGE CPA KANDA YA AFRIKA ZAKUTANA MJINI ZANZIBAR

0

Wajumbe Kamati ya Wawakilishi wa Kanda Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Bernard Sibalatani (katikati) wakati wa kikao kilichofanyika leo Septemba 1, 2019 katika hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa Mjini Zanzibar.

Mwenyekiti wa kamati ya Fedha na Mipango Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika, Mhe. Elijah Okupa (katikati) akiongoza kikao hicho kilichofanyika leo Septemba 1, 2019 katika hoteli ya Madinat Al Bahr Mjini Zanzibar. Kushoto ni Spika wa Bunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Kampuni ya uwekezaji CPA Kanda ya Afrika

Mhe. Job Ndugai na Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati ya Marekebisho ya Sheria Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika walipokaa leo Septemba 1, 2019 katika hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa Mjini Zanzibar. Kushoto ni Mjumbe wa kamati na Naibu Spika wa Bunge la Afrika ya kusini, Mhe. Lechesa Tsenoli na Mwenyekiti  wa kamati ya Wawakilishi wa Kanda Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, Mhe. Bernard Sibalatani