Home Mchanganyiko IGP SIRRO AKUTANA NA IGP WA SUDANI

IGP SIRRO AKUTANA NA IGP WA SUDANI

0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil  Mohamed Ahmed, akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambayo imelenga kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Sudani.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil  Mohamed Ahmed, wakati akitoa hotuba mbele ya Makamishna na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi hilo (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili ambayo imelenga kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Sudani.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akipokea zawadi kutoka kwa  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil  Mohamed Ahmed, ambaye yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, ziara ambayo imelenga kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Sudani.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil  Mohamed Ahmed, wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishna na Maofisa Wakuu Waandamizi baada ya kumaliza kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo leo Jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi Nchini.