Home Mchanganyiko KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO MKURANGA KUONDOA TATIZO LA UKOSEFU WA SOKO KWA...

KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO MKURANGA KUONDOA TATIZO LA UKOSEFU WA SOKO KWA WAKULIMA-NDIKILO

0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
MUHOGO uliokuwa ukiozea mshambani na kukosa soko la uhakika wilayani Mkuranga na maeneo mengine mkoani Pwani ,sasa unakwenda kupata soko la uhakika katika kiwanda cha kuchakata mhogo kilichopo Mkenge kata ya Veta wilayani hapo.
Inadaiwa kwamba ,uzalishaji wa muhogo mkoani humo ni tani 900,000 hadi milioni 1.2 hivyo kuna kila sababu uzalishaji ukaongezeka ili kunufaika na kiwanda hicho.
Akihimiza kilimo hicho ,mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ambae anaendelea na ziara yake ya awali ya kuweka mawe ya msingi katika baadhi ya viwanda ,alisema soko la muhogo lilikuwa duni na wakulima walikuwa wakilima kwa wingi bila kupata faida.
“Kiwanda hiki kitatoa ajira,pia bei ya mhogo itakuwa yenye tija kwakuwa watatumia kupima kwa mzani, kwasasa bei haitabiliki ikiwa lumbesa 60,000 hadi 80,000 ,suzuki 300,000 ambapo kwa hali hiyo ni bei inayomlalia na kumnyonya mkulima huyu wa Mkuranga”alifafanua Ndikilo.
Hata hivyo alieleza ,moja ya malengo ya ziara yake ni kudhihirisha Pwani inakwenda kuwa ukanda wa viwanda pamoja na kuithibitishia Dunia kwamba Tanzania ni eneo linalovutia kwa viwanda.
Nae mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ,mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno alimuelekeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo na wataalamu wa kilimo waende vijijini kutoa elimu juu ya kilimo cha kisasa.
“Tumejifunza kupitia zao la korosho ,sasa mazao yote yaliyopata dawa ya kumkomboa mkulima yatolewe elimu kwa wakulima husika”alisisitiza Maneno.
Awali mhasibu wa kiwanda cha Tanzania Huafeng agriculture development Ltd,Leonard Jabee ,alieleza kiwanda kinamilikiwa na wachina ,kilianza ujenzi march 2019 na utakamilika mwishoni mwa mwaka huu,utagharimu bilioni 9.1.
Alielezea, wataanza kutengeneza vipande vya mhogo na kisafirisha China kisha kuzalisha wanga na kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 200 kwa siku kupitia Amcos za wakulima huku wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme.
Meneja wa Tanesco wilayani Mkuranga, Octavian Mmuni alisema , mwekezaji aliomba tariff II ,mkandarasi ameanza kazi ya kutandaza nyaya na nguzo lakini kazi haijakamilika.