Home Burudani Bella apeleka usiku wa masauti Nefaland Jumamosi

Bella apeleka usiku wa masauti Nefaland Jumamosi

0

***************

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam.  Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi nchini, Christian Bella na bendi yake ya Malaika, wameibuka na wimbo mpya ujulikanao kwa jina la Pacha ambao utatambulishwa Jumamosi kwenye hotel ya Nefaland ya Magomeni Kagera.

Bella ambaye alianza kutamba na wimbo wake, Yapo Wapi Mapenzi akiwa na bendi ya Akudo Impack, ameweza kuliteka soko la muziki wa dansi kwa nyimbo zake mbalimbali ambazo bado zinapendwa katika muziki wa dansi.

Nyimbo hizo ni Nani Kama Mama,  Nishike, Nashindwa, Msaliti, Usilie, Niende Wapi, Nakuhitaji, Rudi, Pambe na Boss ambaye alimshirikisha mrembo, Hamisa Hassan Mobetto.

Mbali ya nyimbo hizo, pia Bella ameweka historia katika muziki wa dansi nchini kwa kuweza kumshirikisha mwanamuziki nyota barani Afrika, Ngiana Makanda maarufu kwa jina la Werrason katika wimbowake wa Moyo.

Pia Bella ameweza kumshirikisha nyota nyingine ya muziki Wa dansi, Fally Ipupa ujilikanao kwa jina Starehe. Mbali na Fally Ipupa na Werrason, Bella pia amemshirikisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, John Makini katika wimbo wake wa Niende Wapi.

Mratibu wa onyesho hilo, Bakari Seif alisema kuwa onyesho hilo litaanza saa 2.00 jioni ili kutoa nafasi kwa mashabiki wa muziki wa dansi nchini kupata burudani inayoendana na kiingilio chao.

Alisema kuwa wanatarajia kupata shoo yenye ubora wa aina yake kwani Bella na wanamuziki wenzake wamejiandaa vilivyo.

“Hili ni onyesho maalum kwa mashabiki wa muziki wa dansi ambao wamekuwa wakimsubiri kwa hamu Christian Bella na bendi yake ya Malaika. Kwa mara ya kwanza, Bella ataimba nyimbo zake zote anazotamba nazo,” alisema Seif.