Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya wiki 3 ya usalama Mahali pa kazi na kuwahimiza kutumia maarifa hayo ili kuleta tija katika uzalishaji
************
NA EMMANUEL MBATILO
WAKALA wa usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) wafanyakazi wanahitaji ongezeko la mafunzo ya mahali pa kazi kwa kiwango Cha hali ya juu nchini.
Akizungumza na waandishi wahabari Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda alipokua akihitimisha mafunzo ya kozi ya Taifa ya usalama na Afya Mahali pa kazi (National occupational safety and Health course-) amesema kozi hiyo imetolewa kwa wiki tatu mfululizo katika ofisi za (OSHA) Kinondoni jijini Dar es salaam.
Aidha,Mwenda amefafanua kuwa jumla ya washiriki 107 kutoka taasisi, makampuni,mashirika na watu binafsi kutoka mikoa mbalimbali kote nchini.
“Kozi hii tulikua tunaitoa mara kwa mwaka lakini kutokana na uhitaji wa mafunzo hayo kuongezeka tumelazimika kutoa kwa awamu nne kwa mwaka,”
Mwenda aliongezea kuwa kimsingi kumekua na mwamko mkubwa sana miongoni mwa taasisi za umma, makampuni binafsi na mtu mmoja mmoja ambao wanafika ofisi za osha kupata mafunzo hayo muhimu kwa ajili ya kuandaa wataalam wa kusimamia masuala ya usalama na Afya katika sehemu za kazi.
Pia ametoa wito kwa wahitimu wa mafunzo hayo kuzingatia na kutumia maarifa waliopata katika kuleta mabadiliko chanya kwenye maeneo ya kazi hususan katika kuboresha mazingira ya kazi ili kuongeza tija katika uzalishaji.Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo amesema ni muhimu sana kwa watanzania wote kuimarisha masuala ya afya na usalama katika maeneo ya kazi.