Home Mchanganyiko MHEA KUWAFUNGUA MACHO WANANCHI NJOMBE KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

MHEA KUWAFUNGUA MACHO WANANCHI NJOMBE KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

0

**********

NJOMBE

Wakazi wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wamepongeza jitihada za  shirika lisilo la kiserikali la Mlangali helth Enviromental Association MHEA kwa kuanza kutoa elimu kwa wananchi wa kata ya Ulembwe na Makoga wilayani Wanging’ombe Mkoani Njombe ili kuwajengea uwezo wa kufatilia taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika vijiji vyao.

Wananchi hao akiwemo Fausto Chaula wamesema hatua hiyo imesaidia kuwajengea uelewa na uwezo katika kufatilia mienendo na matumizi ya fedha za umma katika miradi ya maendeleo iinayotekelezwa katika maeneo yao kwa kuwa kumekuwepo na ripoti nyingi za wakaguzi ambazo zinazonyesha ubadhilifu katika utekelezaji wake jambo ambalo ni gumu kujulikana kwao

Aidha wamesema itasaidia kudhibiti wizi na mianya ya rushwa katika utangazaji wa tenda na katika nyakati za makubaliano ya kandarasi hatua ambayo itakuwa na matokeo chanya kwa jamii nyingi za kitanzania

Mansuli Ngenzi na Atijala Pazi Katika hatua nyingine watendaji walioshiriki katika mafunzo hayo wamesema elimu hiyo mbali na kuwajnegea uwezo na ufahamu lakini pia itahamasisha wananchi kujitokeza katika mikutano ya kijiji ambako hujadiliwa masuala yote ya maendeleo.

Awali akizungumza wakati utoaji wa elimu hiyo mkurugenzi wa shirika la MHEA Edward Wella anasema mwananchi ndiyo mlinzi wa kwanza wa miradi na fedha za serikali hivyo kujengewa uwezo na uelewa katika usimamizi wa miradi hiyo utasaidia kuokoa fedha za umma na kudhibiti mianya ya rushwa.