Home Michezo NASSIBU RAMADHANI, TONNY RASHIDI KIDUNDA WATAMBA KATIKA NDONDI

NASSIBU RAMADHANI, TONNY RASHIDI KIDUNDA WATAMBA KATIKA NDONDI

0

Mkuu wa mafunzo na utendaji kivita wa jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Alfred Kapinga  ( Wakwanza kushoto ) Akimvisha Mkanda wa Ubingwa Afrika mashariki na kati bondia Tonny Rashid aliyeshinda baada ya Kumpiga Haidary Mchanjo  katika pambano lililofanyika Club 361 Mwenge Jijini  Dar Es salaam.

Mabondia wa kulipwa Nassibu Ramadhani na Issa Nampepece wakitifuana wakati wa Mchuano wa Ubingwa Afrika mashariki na kati katika Ukumbi wa 361 Mwenge Bondia Nassib Ramadhani aliibuka Mshindi.

Bondia haidary Mchanjo akimtupia konde Bondia Mwenzie Tonny Rashidi katika Mpambano wa kuwania ubingwa Afrika mashariki na kati Tonny Rashidi aliibuka na ushindi kaptika mpambano huo uliofanyika Club 361 Mwenge.

***************

Mabondia Nassibu Ramadhani na Tonny rashidi wamefanikiwa kutawazwa rasmi mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati katika Mpambano wa kuvutia uliofanyika Jumamosi katika Ukumbi wa 361 Mwenge Jijini  Dar es Salaam.

Katika Mpambano wa Kwanza Nasibu Ramdhani alishinda kwa Pointi  99/91 jaji wa pili 100/90 jaji wa Tatu 99/91  baada ya Mchuano Mkali wa Vuta Nikuvute uliowapelekea kumaliza Raundi zote 10 za Mchezo huku mashabiki wakishuhudia Ngumi za Kuvutia za kila mmoja kumuwinda mwenzie.

Mara baada ya Mpambano huo Nassibu Ramadhani alisema mpinzani wake Issa Nampepeche ni Bondia Mzuri na alitumia Mbinu za kutoka ndio ambazo zilimfanikisha kumaliza Mpambano huo kwa Rundi zote 10.

Naye Bondia Issa Nampepeche alisema  Mpinzani wake alikuwa Mzuri zaidi hivyo anaenda kujipanga upya baada ya kupoteza mchezo huu na anaimani kufanya Vizuri katika Michezo mingine inayofuata.

Katika Mpambano mwingine Bondia Tonny Rashidi aliibuka na Ushindi kwa pointi toka kwa Majaji Wote Watatu ambapo walimpa 97 kwa 93 jaji wa pili 98/92 na Jaji wa Tatu 99/91  Dhidi ya Haidary Mchanjo baada ya kumalizika kwa raundi 10 katika pambano ambalo lilikuwa na hamasa kubwa ya kutakiwa kupatikana kwa mbabe baada ya pambano la Awali kumalizika kwa sare.

Naye Bondia wa  Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Selemani Kidunda alidhihirisha Ubabe wake baada ya kushinda kwa KO katika Raundi ya Kwanza ya mchezo Sekunde ya 45  baada ya kumtwisha Konde bondia Nassoro Hussein.

Mchezo mwengine

Katika Ngumi za wazi  Mabondia wa JWTZ waliokuwa wakijipima Uwezo kwa ajili ya kujiandaa na Mashindano ya Dunia ya Majeshi Nchini China  Bondia George Costatino alimshinda  Bondia Osama Araba wa  Jeshi la Anga ,Ismali Galiatano alimshinda kelvin kipinge, Fabian  Gaudence alishinda  kwa Pointi Dhidi ya Athanas Ndigaya.

Katika mchezo mwingine Alex Michael alishinda kwa KO Raundi  ya tatu Dakika ya pili  dhidi ya Mussa Ally  na Kassim Mbundwike naye alishinda kwa   KO raundi ya kwanza Sekunde ya 30 dhidi ya Julius Nickson wa Jeshi la Anga na Bondia  Mwanmke Irene Kimaro alimtwanga Stumai Muki kwa Pointi.

Mgeni rasmi katika Mpambano huo mkuu wa mafunzo na utendaji kivita jeshini Meja  jenerali Alfred Kapinga alisema huu ni mwanzo lakini wanatarajia kuwa na mapambano mngi hivyo wadau wa ngumi watarajie Mengi
” Nimefarijika na mwitikio wa Watu waliojitokeza na wadau waliotuunga mkono kufanikisha hili tutaendelea na jitihada za kukuza mchezo huo wa Ngumi na kuwapa heshima na Burudani wananchi kufuatia mapambano mbalimbali watakayocheza mabondia wa JWTZ.
Katika Mapambano hayo yaliyotanguliwa na ,mapmbano ya Mieleka ambayo pia yalivutia watu wengi na wadau mbali mbali kuomba mapamnbano zaidi kuandaliwa  kama ilivyo kwa mpambano haya  yaliyodhaminiwa na SmartGin , Kiwango Security  na Resolution Insurance ambao watakabidhi kadi za Bima ya Afya ya Mwaka mmoja kwa Mabondia Walioshinda Ubingwa Afrika Mashariki na Kati.