Home Mchanganyiko ‘BE THE COACH ’ YA  TBL  YANUFAISHA VIJANA WA KITANZANIA

‘BE THE COACH ’ YA  TBL  YANUFAISHA VIJANA WA KITANZANIA

0

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TBL,  Philip Redman, akiongea na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya miezi mitatu ya Be The Coach Program, yaliyoandeshwa na TBL

Mmoja wa wahitimu wa programu ya Be The Coach ya TBL, Lawrence Isaac akieleza jinsi alivyonufaika na mafunzo hayo

Meneja Vipaji wa TBL,  Kisa Mwasomola, akiongea wakati wa mahafali hayo

Mmoja wa wakufunzi katika programu hiyo,Costantine Magavilla,akiongea wakati wa mahafali hayo

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TBL,  Philip Redman akifurahi pamoja na Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi (Katikati) na Mkufunzi Costantine Magavilla.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TBL,  Philip Redman,  akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu 

 ……………………

Programu ya mafunzo ya  ‘Be the Coach’ ya kampuni ya TBL , inayolenga kuwapatia vijana wa kitanzania elimu ya kujitambua imeanza kuonyesha mafanikio ambapo wahitimu wa awamu ya kwanza wameeleza kuwa wamefanikiwa kujua mambo mengi ambayo hawakuyajua kwenye vyuo walivyopitia yatakayowasaidia kukabiliana na shughuli zao katika Maisha ya kila siku.

Programu hii ya miezi 3 kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18-26, kwa  awamu ya kwanza imefanyika Dar es Salaam, inalenga kuwapatia elimu ya kujitambua kwa ajili ya kutumia maarifa na vipaji walivyo navyo kuweza kupata mafanikio katika maisha yao na inaendeshwa na wafanyakazi wa TBL kwa njia ya kujitolea.

Katika mahafali ya kwanza iliyofanyika katika ofisi za  Makao Mkuu ya kampuni mwishoni mwa wiki, baadhi ya wahitimu walieleza kuwa  wameweza kujifunza mambo mengi katika kipindi cha muda mfupi ambayo hawakuyajua hapo awali ambayo wanaamini yatawasaidia kupata mafanikio ya kimaisha.

“ Tunajivunia kupata nafasi ya kushiriki  mafunzo haya yanayoendeshwa na wafanyakazi wa TBL kwa kuwa yametuwezesha kujua mambo mengi, ikiwemo jinsi ya kuanzisha shughuli zetu na kuzisimamia kwa ufanisi badala ya kutegemea kuajiriwa, kujiamini, kuwa na nidhamu katika kazi na biashara na mengineyo mengi.Naomba kampuni iendelee kutoa mafunzo haya na kuhakikisha yanawafikia vijana wengi zaidi nchini ”,alisema  Lawrence Isaac mmoja wa wahitimu kwa niaba ya washiriki wenzake.

Kampuni ya TBL chini ya kampuni mama ya kimataifa ya AB InBEV inayo sera ya ‘Kujenga Ulimwengu Maridhawa’ ambayo inalenga kuleta mabadliko  chanya  na maendeleo endelevu katika maeneo yote inakofanyia biashara zake, kama ambavyo wafanyakazi wake wamejitolea kutumia muda wao na elimu yao kuwapatia maarifa vijana wa kitanzania waliohitimu mafunzo haya.
Programu kama hii inadhihirisha jinsi kampuni ya TBL inavyoendelea kufanya uwekezaji ambao unatoa mchango wa ukuzaji wa  uchumi na jamii  nchini.