Home Michezo BALINYA AIBUKA SHUJAA, YANGA KUIONDOA TOWNSHIP ROLLERS LIGI YA MABINGWA AFRIKA

BALINYA AIBUKA SHUJAA, YANGA KUIONDOA TOWNSHIP ROLLERS LIGI YA MABINGWA AFRIKA

0

**********

 
NA EMMANUEL MBATILO

Mshambuliaji wa nchini Uganda anaeichezea klabu ya Young Afrika Juma Balinya amefanikiwa kuiwezesha klabu hiyo kutinga hatua inyofuata baada ya kufanikiwa kupachika bao moja na kuiwezesha timu yake kusonga mbele kwa idadi ya mabao 2:0 dhidi ya Township Rollers katika Uwanja wa Taifa mjini Gaborone, Botswana.

Balinya alifunga bao hilo pekee kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 41 na kuitanguliza klabu yake ikiwa mbele kwa bao moja mpaka mapumziko.

Kwa kwa matokeo hayo, Yanga SC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita mjini Dar es Salaam na itamenyana na Zesco United ya Zambia iliyoitoa Green Mamba ya Eswatini kwa jumla ya mabao 5-0, ikishinda 2-0 ugenini na 3-0 nyumbani.