Home Mchanganyiko WATANZANIA WAELEKEA ISRAEL KUJIFUNZA UTALII NA TEKNOLOJIA 

WATANZANIA WAELEKEA ISRAEL KUJIFUNZA UTALII NA TEKNOLOJIA 

0
Mratibu wa Safari hiyo Padre Melodis Mlowe wa Jimbo Katoliki la Njombe 
Haryson Chanjo kutoka kamapuni ya Exellence Guide ni miongoni mwa waratibu wa safari ya kidini ya utalii kuelekea ISRAEL
Mmoja wa wasafiri akiwa tayari uwanja wa Kimataifa KIA akiwa ameambatana na binti yake 

Baadhi ya Watanzania 64 amabao wameshaanza safari kuelekea nchini Israel kwaajili ya safari ya Kidini pamoja na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Teknolojia.

Baadhi ya Watanzania 64 wakiwa uwanja wa Kimataifa wa ambao tayari kwa safari kuelekea nchini Israel kwaajili ya safari ya Kidini pamoja na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Teknolojia.

Baadhi ya Watanzania 64 ambao wameshaanza safari kuelekea nchini Israel kwaajili ya safari ya Kidini pamoja na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Teknolojia.  
Na.Vero Ignatus,Arusha.

 
Zaidi ya Watanzania 64 kutoka Mikoa yote nchini wameondoka kwenda nchini Israel kwaajili ya safari ya kidini pamoja na kujifunza mambo mbalimbali yaTeknolojia pamoja nakutangaza utalii na vivutio mbalimbali vilivyo Nchini.

Akizunguza Mratibu wa Safari hiyo Padre Melodis Mlowe wa Jimbo Katoliki la Njombe amesema kuwa mafanikio ya safari hiyo yanatokana na Balozi wa Tanzania nchini Israel kuwataka watanzania kutumia fursa ya ndege inayowaleta watalii nchini,ili waweze kuitumia kwenda Israel kujifunza kwani bei yake ni nafuu ukilinganisha na bei za ndege nyingine.
 

 

\\Kupitia fursa gharama ambayo ilikuwa inasomeka mil 8-9 kwa mashirika na makampuni mengine kupitia program hii gharama ni pungufu sana kwasababu dola wanayolipa ni 1390 kwa tikati ya ndege malazi chakkula na na safari nzima kwenda na kurudi kwa siku saba ni gharama pungufu kuliko gahrama yeyote ile.// Padre Mlowa amesema lengo kuu ya safari hiyo ni watanzania kwenda nje ya nchi kujifunza,yakiwemo mambo mengi ambayo wanatakiwa kujifunza ikiwemo ujasiri,teknolojia na maendeleo,amesema Israel ndiyo nchi sahihi kwani uoto wa nchi hiyo ni mawe mchanga pamoja na jangwa ila ndiyo nchi yenye mafanikio makubwa.

Akizungumza wakati  wakianza safari
Padre amesema katika matatizo ya uoto wa nchi hiyo ya Israel, wameigeuza kama
fursa kwao hivyo wao kama watanzania wanakwenda siyo kwaajili ya kutalii peke yake bali kujifunza fursa mbalimbali na kutangaza Utalii wa Tanzania.


 //Hakuna haja ya Nchi ya Tanzania kuendelea kuwa maskini wakati tunazo fursa nyingi ukitofautisha na Israel,wao changamoto kubwa waliyonayo ni ardhi yao kubwa ni mawe,mchanga na jangwa ila sisi tunakwenda kujifunza wamewezaje kufanikiwa//alisema padre Mlowa.


Amewataka watanzania kutoka kwaajili ya kujifunza katika
nchi mbalimbali kwaajili ya kupata mtazamo chanya kwaajili ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Haryson Chanjo kutoka kamapuni ya Exellence Guide ni miongoni mwa waratibu wa safari ya kidini ya utalii kuelekea ISRAEL amesema kuwa wameitumia fursa hiyo ya ndege inayoleta watalii kutoka Israel kuja kutembelea mbuga za wanyama nchini ambayo wanafanya mabadilishano ya wao kuja na watanzania kwenda kujifunza mambo mbalimbali kwani wao wanapata biashara na Tanzania vilevile.


Amesema safari kama hizo lengo kubwa ni kutangaza utalii wa taifa katika masoko mapya kwani zipo nchi nyingi duniani zinahitaji kujua Tanzania kuna vivutio mbalimbali ,ikiwemo mlima Kilimanjaro,hifadhi na vivutio vingi vya asili.
 \\Novemba 12 mwaka huu tutakuwa na ndege nyingine inaondoka kuelekea Israel, safari nyingine Mwezi wa kumi na moja mwakani tutaanza mara tu baada ya
pasaka tutakuwa na mtiririko wa safari kwani mwitiko mkubwa sana kwa
watanzania ila changamoto kubwa ni muda wa maandalizi umekuwa mdogo sana na
vithibitisho vyote vinavyohusisha nyaraka paspoti na na viza //Alisema Hurryson
Amesema kuwaamefurahi kuona Tanzania ina balozi nchini
Israel kwani imekuwa rahisi kwa watanzania kupata nafasi  ya kwenda Israel
vilevile wanaomba Israel iweze kufungua ofisi ya ubalozi nchini ili iwe rahisi
kwa watanzania kupata viza kirahisi ilikuepusha watanzania kwenda kutafuta viza
nchini Kenya.
 
Kuna gharama ya watanzania kwenda Kenya kutafuta viza
na kurudi Tanzania tena kampuni ya Exellent Guide watoe huduma hiyo kwa wingi
zaidi ili watanzania wengi waweze kunufaika na huduma hiyo sambamba na kutangaza utalii katika masoko mapya kama Asia,Amerika na nchi nyingine ambazo zinahitaji kuifahamu Tanzania.

 

 

 

Aidha Watanzania waliosafiri kwenda nchini Israel wametoka katika mikia ya Mwanza Dar es salaam,Iringa Njombe,Musoma Dodoma,
Njombe,Kilimanjaro,Arusha,Tanga,ambapo safari hizo zitakuwa endelevu.