Home Mchanganyiko MAHAKAMA YASHUSHA RUNGU KATIKA KIWANDA CHA CHAI IKANGA KWA KUKWEPA KODI

MAHAKAMA YASHUSHA RUNGU KATIKA KIWANDA CHA CHAI IKANGA KWA KUKWEPA KODI

0

NJOMBE

Mahakama ya mwanzo katika kijiji cha Lupembe wilayani Njombe imetoa siku 45 kwa muwekezaji wa kiwanda cha chai Ikanga kuilipa halmashauri ya wilaya ya Njombe kiasi cha mil 19 baada kujiridhisha kwamba muwekezaji wa kiwanda hicho amekwepa kulipa ushuru wa serikali katika uzalishaji wa majani ya chai katika kipindi cha miezi tisa pamoja fedha kiasi cha mil 3 kutokana na ukwepaji kodi ya pango la nyumba ya halmashauri tangu julai 2018 hadi march 2019 na kuisababishia hasara serikali.

Hukumu ya kesi hizo imetolewa na hakimu Godfrey Msemwa katika mahakama ya mwanzo ya kijiji cha Lupembe ambapo katika shauri la kwanza la kesi ya madai no 3 ya 2019 imedaiwa kwamba kiwanda cha Ikanga kimekwepa kulipa ushuru wa serikali wa uzalishaji wa majani ya chai wa zaidi ya mil 19 jambo ambalo ni kosa ni kosa la kisheria.

Katika kesi ya pili ya madai no 4 ya mwaka 2019 kiwanda Ikanga kimebainika kukwepa kulipa deni la kodi ya pango la nyumba ya halmashauri katika kijiji cha lupembe barazani kwa zaidi ya miezi 6 na kuikosesha fedha ya ushuru serikali kiasi cha shilingi mil 3

Awali akitoa hukumu ya kesi no 3 na na 4 za madai za mwaka 2019  hakimu Godfrey Msemwa amesema mahakama imejiridhisha kwamba madai yaliyotolewa na mdai ambaye ni halmashauri ya wilaya ya njombe ni halali na kwamba mdaiwa ambaye ni kiwanda cha Ikanga amekubali kulipa fedha yote katika kipindi cha siku 45 pamoja na gharama nyingine za msingi

Nje ya mahakama mwakilishi wa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya njombe lukero mshaura ambaye ni afisa habari katika halmashauri hiyo amezungumzia hukumu iliyotolewa na mahakama pamoja na sababu za kufunguliwa kwa kesi hizo mbili  huku nae mwakilishi wa kiwanda cha Ikanga akigoma kuzungumza chochote kuhusu uamuzi wa mahakama kwa madai kwamba sio msemaji wa kiwanda.

Katika hatua nyingine mahakama imeamuru kiwanda kulipa gharama zote uendeshaji wa kesi, fedha ya ushuru pamoja na kodi ya pango katika kipindi cha siku 45 .