Home Mchanganyiko MAAFISA ELIMU WAMETAKIWA KUSIMAMIA SHULE BINAFSI

MAAFISA ELIMU WAMETAKIWA KUSIMAMIA SHULE BINAFSI

0

Na.Farida Saidy,Morogoro

Naibu waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Mwita Waitala amewataka Maafisa elimu kote Nchi kusimia shule zote bila ya kubagua shule ya umma au ya mtu binafsi katika kutekeleza na kusimamiasela ya elimu nchini. 

Naibu Waziri Waitala ameyasema hayo Mkoani Morogoro katika ufunguzi wa kongamano la walimu wa shule binafsi nchini lililoandaliwa  na chama cha TPTU ambacho kinawsimamia walimu hao,ambapo amesema kuwa maafisa elimu wanajibu wa kusimamia na kufuatilia mienendo ya shule zote bila ya kubagua shule ya umma au binafsi.

Aidha waitala amekemea vitendo vya wakuu washule kupandisha ada ya masomao pasipo kukubaliana na wazazi wa husika wa mtoto.

 Unakuta mwalimu amekaa na wazazi fulaani katika kikao halafu anaandika kwenye muktasari kuwa tumekubaliana katika kikao cha wazazi ada itakuwa hii.amesema waitala

Unamkuta mtoto amesoma katika shule x kuanzia dalasi la kwanza hadi la saba harafu badaye mwalimu anamfukuza mtoto huyo kwa sababu tu hajaripa fedha ya mtihani fulani,kiukweli tuwe na roho za kiutu basi.amesema waitala   

Katika hatua nyingine Waitala amewataka wamiliki wa shule binafsi kuheshimu mikataba ya kazi kwa  waajiri wao hususani walimu pamoja na ile ya wazazi wa wanafunzi, ambapo amesema mala nyingi kumekuwa na mkanganyiko wa ada katika shule za binfsi. 

Kwa upande wake katibu wa chama cha walimu wa shule za binafsi (TPTU) Bwana Julias Mabula ameimba serikali kuangalia kwa makini swala la shule binafsi kuajiri walimu ambao sio raia wa watanzania kwani wengi wao wamekuwa hawana vibali vyakuishi na kufanya kazi nchini.