Home Mchanganyiko Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi....

Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe.

0

***************

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Prof.Florens Luoga amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya ya Afrika (Africa Group 1), Bi.Anne Kabagambe ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Gavana Luoga amemwelekeza Bi.Kabagambe hatua mbalimbali ambazo BoT inachukua kuhakikisha kuna ukuaji wa uchumi,kuimarisha sekta ya mabenki,mifumo ya malipo na huduma jumuishi za kifedha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Kuu ya Dunia aliipongeza BoT kwa hatua mbalimbali inazochukua kutekeleza sera ya fedha na na kueleza utayari wa Benki ya Dunia kushirikiana katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Manaibu Gavana wa BoT, Dkt.Yamungu Kayandabila na Dkt.Benard Kibesse na Mshauri Mwandamizi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji huyo, Bw.Zarau Kibwe, walihudhuria mazungumzo hayo.