Home Mchanganyiko WADAIWA SUGU NYUMBA ZA TBA DODOMA WAANZA KUONDOLEWA

WADAIWA SUGU NYUMBA ZA TBA DODOMA WAANZA KUONDOLEWA

0

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) imewatolea uvivu wapangaji wake ambao wamekuwa sugu kwa kutolipa kodi ya pango kwa wakati hali iliyosababisha kuwatolea vitu vyao nje kutokana na kudai zaidi ya bil 1.5 huku wabunge wakitajwa kuhusika.

Pia wastaafu nao watakiwa kuhama katika nyumba hizo kwani TBA wanaamini kuwa mtu akishastaafu anauwezo wa kuwa na nyumba yake mwenyewe.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Kaimu Meneja Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma Helman Tanguye  baada ya kufanya zoezi hilo alisema kuwa wadaiwa hao wamelimbikiza madeni yao kwa miaka 10 sasa.

Alisema kuwa TBA imekuwa ikidai fedha nyingi sana na hasa katika mkoa wa Dodoma kwa wafanyakazi wa serikali na taasisi mbalimbali za serikali ambazo wamezipangisha.

“Mpaka sasa tunadai zaidi ya bil 1.5 hivyo lengo kuu la TBA ni kuwaondoa wale watu walioshindwa kulipa kodi ya pango kwa wakati ili watu wanaohamia kutoka mikoa ya Dar es salaam na mingineyo nao waweza kupata nafasi”alisema Tanguye.

Akizungumzia zoezi zima walivyolianza alisema kuwa “tumelianza jana baada ya kufanya taratibu zote za kisheria na mikataba inavyosema kwahiyo tuliwapa notes ya siku 30 badaye tukaongeza Siku 14 lakini zilivyokwisha tulichukua vyombo ambavyo vinatambulika na mahakama ili tuweze kuwaondoa.

Alisema kampuni wanayoitumia katika zoezi zima la kuwatolea watu vitu vyao nje ni Yono Auction Mart ambayo wamekuwa wakiitumia mara kwa mara katika shughuli zao.

Wakati huo huo Tanguye alisema kuwa TBA ukiacha kazi yake yakujenga nyumba lakini pia inamiliki nyumba ambazo imewapangisha wananchi,taasisi,makampuni ,na wabunge lakini chakushangaza watu hao wamekuwa wakikaidi kulipa hata baada ya kupewa notes ya mwezi mmoja”

“Zoezi hili hapo awali lilifanyika jijini Dar es salaam  lakini kwa sasa limehamia jijini Dodoma ambapo litakuwa endelevu kwa mikoa yote nchini”alisema.

Pia wapangaji amabao hawajahuisha mikataba yao ya mwaka basi nao wanahusika kuondolewa kwani wanaonyesha kyuwa hawana nia ya kuishi katika nyumba hizo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Afisa miliki fredy mangala alisema kuwa mnamo juni 30 waliwasisitizia kuwa wametoa notes hivyo wanaodaiwa waende wakalipe lakini baada ya kuona wamekaidi agizo hilo wakaona bora kuchukua hatua hizo za kuwatolea vitu vyao nje.

“Wale wote wanaodaiwa na waliopata notes walipe madeni hayo kama inavyotakiwa hivyo zoezi hilo litakuwa endelevu kwani sheria inakataza kwa mtumishi wa umma kuwa na madeni.

Alisema kuwa fedha zaidi ya bil.1.5 ni nyingi sana kwani wangeweza kuzitumia ongeza nyumba nyingine eneo la Nzuguni ambapo wana eneo la hekali 630.

Mangala alisema kuwa wabunge nimiongoni mwa watu wanao daiwa hivyo wanachotakiwa ni kutekeleza majukumu yao kama mikataba inavyosema nakusema kuwa wao kama wakala wataendelea kutekeleza wajibu wao.

“Lakini endapo pia kuna mbunge atafikia kiwango cha kutolewa basi itabidi atolewa ingawa kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakijitokeza na kutuonesha ushirikiano”alisema.

Hata hivyo Malanga alisema kuwa mikataba hiyo inaelezea mtumishi akistaafu,akifariki au kuhamishwa mkoa mwingine inabidi kuachia nyumba ,hivyo katika zoezi hilo wanalolifanya pia wanaangalia watu hao.