Home Uncategorized MWANAMKE ANAYEDAIWA MCHAWI AZUA TAHARUKI IRINGA

MWANAMKE ANAYEDAIWA MCHAWI AZUA TAHARUKI IRINGA

0

Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi

TAHARUKI na bumbuwazi imewakuta wakazi wa Isele Ilula Wilaya ya Kilolo na Mkoa wa Iringa baada ya mwanamke anayedaiwa Mshirikina kukutwa kwenye paa la Nyumba la Mchungaji, Jeremia Charles usiku wa saa 11 alfariji.

Akuzingumza na Waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Juma Bwire alisema mwanamke huyo aliyetambulika kama Kabula Masunga, umri 41, mpagani mkazi wa Morogoro alikutwa akiwa katika mazingira hayo amejifunga mavazi ya rangi nyekundu na nyeusi lakini kifua aliacha wazi.
“Aidha alikutwa na ungo uliyofungwa kitambaa ya rangi nyeusi na nyekundu.

Alisema mwanamke huyo alikutwa akiwa na Pembe ya Ng’ombe na alijifunga hirizi mikononi.

Aliongeza kuwa mwanamke huyo alikuwa na wenzake wanne ambao walikuwa wakisafiri kwa kutumia Ungo.
Aliongeza kuwa wanaendelea kumhoji zaidi ili kufahamu lengo la kufanya ushirikina huo