Home Siasa CCM CHAWATOA HOFU MADEREVA BAJAJI NJOMBE

CCM CHAWATOA HOFU MADEREVA BAJAJI NJOMBE

0

**************

NJOMBE

Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Kimesema Hakiko Tayari Kuona Madereva Bajaji Wananyanyaswa Kwa Namna Yoyote Ile Ilihali Wanafuata Sheria za Nchi Pindi Wawapo Barabarani.

Taarifa Hiyo Imetolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe Ndugu Erasto Ngole Wakati AKizungumza na Madereva Hao Katika Ofisi za CCM Wilaya ya Njombe Ambapo Amesema Atakuwa Nao Bega Kwa Bega Katika Manyanyaso Ambayo Yamekuwa Yakiwapata Kwa Kipindi Kirefu Yanayofanyika na Baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani Ambao Wamekuwa Wakitumia Vyeo Vyao Kuvunja Sheria.

Hata Hivyo Bwana Ngole amewataka madereva hao kuwaunga mkono katika uchaguzi wa serikali za mitaa ujao kwa kuwa mabalozi wazuri ili chama hicho kipate ushindi.

Baadhi ya Madereva Hao Akiwemo Lameck Mgina,Ismail Mwinyimkuu na Abel Sabas Wamewaeleza Viongozi wa CCM Kero Mbalimbali Zinazowakabili Katika Kazi Yao Ikiwemo Tatizo la Miundombinu ya Barabara Pamoja na Kulazimishwa Kufanya Mambo Ambayo Hayawahusu.

Hanaf Msabaha ni Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Ambaye Anawataka Madereva Bajaji Kuendelea Kukiunga Mkono Chama Cha Mapinduzi Kwani Kinaendelea Kutatua Kero na Kuboresha Miundombinu Ambayo Wanalalamikia.