Home Mchanganyiko NGOs 158 ZAONDOLEWA KWENYE REJISTA YA MSAJILI

NGOs 158 ZAONDOLEWA KWENYE REJISTA YA MSAJILI

0

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi Vickness Mayao (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Msaidizi Uratibu na Ufuatiliaji Bi. Grace Mbwilo (katikati) na Bw. Baraka Leornard Mkurugenzi Msaidizi Usajili wakimsikiliza mdau wa NGO aliyefika kupata maelekezo kuhusu uhuishaji wa usajili wa Shirika lake wakati wa zoezi la kusajili NGOs lililohitimishwa mwishoni mwa wiki katika Nyanda za Juu Kusini Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Timu wa wataalam wa usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya- Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii wakihudumia wadau waliofika kuhuisha usajili wao zoezi la usajili wa mashirika hayo lilolofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Sekretatieti ya Mkoa wa Mbeya wakitoa ushauri wa kwa wadau waliofika kuhuisha usajili wa mashirika yao wakati wa zoezi la usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserika lilililohitimishwa katika Mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Mkurugenzi Msaidizi Usajili Bw. Baraka Leonard (kulia) akikabidhi cheti cha usajili kwa mmoja wa wadau waliofika kukamilisha usajili wakati wa zoezi la usajili wa mashirika hayo lilohitimishwa mwishoni mwa wiki kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

Mdau wa NGO Bi. Joanitha Mtayobya mkazi wa jijini Mbeya akipokea cheti cha usajili wa Shirika lake kutoka kwa Maafisa Wasajili wa Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati  zoezi usajili wa mashirika hayo lilohitimishwa mwishoni mwa wiki kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

 

Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

*****************

Na Mwandishi Wetu Mbeya

Msajili   wa   Mashirika   Yasiyo   ya   Kiserikali   nchini   (NGOs)   Bi.   Vickness   Mayao ameyaondoa Mashirika zaidi  ya 158  kwenye  Rejista ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Hayo yamesema jijini Mbeya na Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa NGOs kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Grace Mbwilo kwa niaba ya Mkurugenzi na Msajili wa NGOs nchini.

Bi. Grace amesema kuwa katika Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya Mwaka 2002  kama ilivyofanyiwa Mabadiliko  na Sheria  Namba 3 ya Mwaka  2019, imefafanua bayana kuwa jukumu  la kusajili mashirika yanayoendesha shughuli za kijamii, kiutamaduni, kiuchumi, utawala bora, haki  za  kibinadamu na  mazingira   katika  ngazi  ya  jamii  kwa  lengo  la kutogawana faida  na  ambazo hazina mrengo wa  wa  kukuza  biashara, zimeelekezwa kusajililiwa na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs).

“Mashirika   yaliyoondolewa   kwenye   daftari    la   Msajili   wa   NGOs   ni   yale   ambayo yalisajiliwa chini  ya Sheria  ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.  24   ya mwaka 2002 ambayo yanafanya kazi kwa   lengo  la kunufaisha wanachama wake, kugawana faida, yenye   mlengo  wa   dini,  yenye   lengo   la  kukuza   biashara  na   Bodi  za   wadhamini”, alisema Bi. Grace.

Bi. Grace ameongeza kuwa, hatua ya kuyaondoa mashirika haya  kwenye  daftari  la msajili wa NGOs imefikiwa kwa mujibu wa Sheria ya Marekebisho Na. 3 ya mwaka 2019 iliyoanza  kutekelezwa  kuanzia  tarehe 1 Julai  2019.  Kwa mujibu  wa  Sheria,  Mashirika hayo yanatakiwa kwenda kujisajili chini ya Sheria  husika ikiwemo  Sheria  ya Jumuiya za Kijamii(Sura  ya 337), Sheria  ya Munganisho wa Wadhamini(Sura ya 318)  na  Sheria  ya Makampuni (Sura  ya 212), na kwamba inatakiwa kukamilisha zoezi  hili kabla  ya tarehe 01 Septemba,2019.

Ameeleza kuwa wa  kuzingatia ufafanuzi wa  mipaka ya  usajili ulioainishwa na  Sheria  Namba 3  ya Mwaka   2019,  Msajili  wa   Mashirika  Yasiyo  ya   Kiserikali  (NGOs)  anayakumbusha Mashirika yanaofanya shughuli kwa lengo  la kugawana faida, yenye mrengo wa dini na ambayo yana  malengo wa kukuza  biashara, kwamba  mashirika ya aina  hiyo yatafutwa kwenye  daftari  la Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali baada ya kipindi cha  miezi miwili  kuanzia  tarehe  01.07.2019 na  yatahamishiwa  chini  ya  Mamlaka  nyingine  za Usajili kutokana na kukosa sifakuwa NGO.

Katika kuhitimisha zoezi  la usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali liliofanyika Mkoani Mbeya, Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali imewaagiza wadau wa mashirika yote  yaliyosajiliwa kwa  lengo  la kuzalisha faida  na  kugawana faida  kuhakikisha kuwa wanahamisha usajili ili kuhuisha taarifa zao kwa Msajili stahiki.

Hatua  hii imechukuliwa na  Msajili wa  Mashirika Yasiyo ya  Kiserikali katika  hatua ya mwisho   ya   Usajili   wa   Mashirika   hayo   kwa   Kanda   ya   Nyanda    za   Juu  Kusini inayohitimishwa mwisho wiki katika ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya na orodha ya Mashirika 158 yaliyoondolewa kwenye  daftari inapatikana katika tovuti ya Wizara www.mcdgc.go.tzna ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. www.tnnc.go.tz