Home Michezo Simba kumkosa Manula,Azam kumkosa Agrey Moris katika Ngao ya Hisani

Simba kumkosa Manula,Azam kumkosa Agrey Moris katika Ngao ya Hisani

0

*******************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba itawakosa baadhi ya mastaa wao katika mechi ya ngao ya hisani dhidi ya Azam leo,wakiwemo mlinda mlango,Aishi Manula na washambuliaji Ibrahim Ajibu na Wilker Henriue Da Silva.

Hivyo klabu hiyo itamtegemea mlinda mlango namba mbili wa klabu hiyo, Beno Kakolanya kuongoza miamba hiyo ya mtaa wa Msimbazi.

Kwa upande wa klabu ya Azam wakati itawakosa mabeki wake wawili Agrey Morris na  Bruce Kangwa pamoja na kiungo wao Mudathir Yahya.

Azam itaingia katika mchezo huo ikiwa na kambukumbu ya kutoa kipigo kikubwa kwa Namungo cha mabao 8-1 siku ya Alhamisi huku Simba ikitoka sare ya bila kufungana na UD Songo ya Msumbiji.

Ligi kuu Tanzania bara itaanza wikiendi ijayo ambapo timu 20 zitaanza kutupa karata zake huku Simba, Yanga, Azam na KMC hazitaanza kwakua zitakuwa na majukumu ya mechi za kimataifa.