Home Mchanganyiko SERIKALI KUVUNA VIBOKO KATIKA BWAWA LA MILALA KATAVI

SERIKALI KUVUNA VIBOKO KATIKA BWAWA LA MILALA KATAVI

0

Baadhi ya viboko wanaoonekana katika Bwawa la Milala lililopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi

Askari wa Jeshi USU wakipita kwa gwaride mbele ya viongozi mbalimbali katika Kituo cha Mafunzo Mlele

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko akipokea salamu kutoka kwa askari wa Jeshi USU waliohitimu mafunzo

…………………..

Na Mwandishi wetu, katavi      

Wizara ya Mali Asili na Utalii kwa kushirikiana na Taasisi ya Uhifadhi wa wanyama Pori Nchini (TAWA) wamejipanga kuvuna viboko katika bwawa la Milala lililopo katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ambao wamekuwa wakisababisha mauaji ya wananchi pamoja na kuharibu mazao ya wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka bwawa hilo

 

Akizungumza na waandishi wa habari kamishna wa uhifadhi wa TAWA dokta James Wakibara alisema kutokana na kuongezeka kwa shughuli za uhifadhi nchini wanyama wamezidi kuzaliana na hata kuhamia katika mabwawa yaliyochimbwa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu

 

“Wenzetu wa Idara ya Maji walichimba mabwawa kwa ajili ya vyanzo vya maji ambayo baadae wanyama wamehamia na kuzaliana, tatizo kama hili pia lipo katika maeneo ya Meatu na Babati lakini tukumbuke pia kuwa binadamu nao wamezaliana sana na kusogea kuishi katika maeneo ya wanyama pori” alisema Dk. Wakibara…kamishna wa uhifadhi tawa

Amesema kuwa hali hiyo imekuwa ikileta migogoro mikubwa

 

Kuhusu fidia kwa wananchi waliopata madhara kutokana na wanyama hao Dk. Wakibara aliwataka kuwa na subira kwani serikali inatambua madai yao

 

Bwawa la Milala lililochimbwa kwa ajili ya chanzo cha maji Mpanda lina wanyama aina ya viboko zaidi ya sitini ambao wamekuwa wakiharibu mashamba ya wananchi na hata kusababisha mauaji wakati mwingine hali inayolalamikiwa na wananchi mara kwa mara

 

Katika hatua nyingine askari wa wanyama pori waliohitimu mafunzo katika Kituo cha Mafunzo cha Mlele wametakiwa kuwa na nidhamu na maadili ya kijeshi ili kuendelea kutunza hifadhi na mali asili za nchi

Akifunga mafunzo ya askari wa Jeshi USU 280 waliohitimu mafunzo hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Meja Jenerali MstaafuHamis Semfuko amewataka askari hao kuepuka vishawishi vya rushwa

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yameleta mafanikio makubwa katika kupambana na ujangili wa wanyamaporihasa tembo ambapo kwa kipindi cha miezi sita hakuna tembo hata mmoja aliyeuwawa kwa viashiria vya ujangili katika hifadhi yaSelous

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi; mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando amesema juhudi za uhifadhi zimeanza kuonekana katika maeneo mbalimbali hasa katika mapito ya wanyama ambayo yalikuwa yamevamiwa na wananchi ambapo sasa wanyama wameanza kuonekana katika maeneo hayo

Aidha Mhando aliwataka askari hao kuendelea kusimamia sheria za uhifadhi wa misitu na uhifadhi wa wanyama pori kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae