Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI BASHE: BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO (CPB) KUWA KIUNGO...

NAIBU WAZIRI BASHE: BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO (CPB) KUWA KIUNGO WA BIASHARA YA MAZAO YA CHAKULA BAINA YA KENYA NA TANZANIA

0

 

NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema kikao cha kwanza baina ya timu ya
wataalamu wa masuala ya Mazao ya Chakula hapa nchini ikiongozwa na Bodi ya
Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na ya wenzao kutoka Kenya zinakutana hapa
nchini leo Agosti 17, 2019 ili kujadiliana namna bora ya kufanya biashara ya
mazao hayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana usiku Agosti 16, 2019 kwenye ofisi za Kituo cha
Uwekezaji Nchini (TIC), jijini Dar es Salaam, Mhe. Bashe alisema, kikao hicho
ni makubaliano baina ya nchi hizo mbili kukutana na kujadili namna gani
wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao wa Kenya watafanya  biashara ya mazao ya chakula na iwe biashara
endelevu.
“Biashara
tayari imekwisha anza na wakati tunaendelea mpaka sasa wenzetu wa Kenya wamekwishanunua
jumla ya tani 34,000 kupitia kwa wafanyabiashara wetu na biashara hiyo
inaendelea.”
Alifafanua.
Alisema
timu ya wataalamu kutoka Tanzania itaongozwa na watu kutoka Wizara ya Kilimo,
Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na
Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) ili wakae chini na wakubaliane utaratibu wa
namna gani  wafanyabiashara wa Tanzania
na wenzao wa Kenya watafanya biashara ya mazao ya chakula.
“Sisi
Wizara ya Kilimo jukumu letu ni kufanya mambo makubwa mawili, kuhamasisha
uzalishaji wa mazao na kufungua masoko ya wakulima wetu ili waweze kufanya
biashara.”
Alifafanua.
Alisema
katika kikao hicho wametaka mamlaka za viwango za Kenya na Tanzania zijumuishwe
kwenye majadiliano hayo ili wazalishaji wa sembe waliosajiliwa Tanzania waweze
kusajiliwa Kenya Bureau of Standards
ili bidhaa zao ziweze kwenda katika soko la Kenya bila vikwazo vyovyote.
“Tunatengeneza
Government Agreement ambayo itaonyesha mpango kazi (frame work) ya namna
biashara hii itafanyika, tumeshaiteua Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko
ambayo ndiyo itakayokuwa kiongozi msimamizi na kiungo wezeshi katika biashara
hiyo.”
Alibainisha Mhe. Bashe.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (katikati), akiwa kwenye kikao baina ya ujumbe kutoka Kenya na wataalamu kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao MchanganyikoTanzania (CPB) kwenye kituo cha Uewekezaji Nchini (TIC) jijini Dar es Salaam. Timu ya wataalamu kutoka Kenya na ile ya Tanzania zinakutana leo kujadili namna bora ya kuwezesha wafanyabiashara wa nchi hizo mbili kufanya biashara ya mazao ya chakula kwa njia rahisi na rasmi.
 Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Bw. Valerian Mablanketi (aliyesimama), akizungumza kwenye kikao hicho.
 Naibu Waziri Bashe (katikati), na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Bw. Valerian Mablanketi, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kilimo, kutoka Wizara ya Kilimo Nchini Kenya, Bw.Badu Katelo, wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe kutoka Kenya.
Naibu Waziri Bashe, akiwa katika picha ya pamoja kati ya wataalamu wa CPB na ujumbe kutoka Kenya