Home Mchanganyiko ARUMERU KUMALIZA KERO YA BARABARA

ARUMERU KUMALIZA KERO YA BARABARA

0
Na Woinde Shizza ,Arusha
 kero ya ubovu Wa Barabara iliyokuwa ikiwakabili wananchi Wa Arumeru imeweza kutatulika Mara baada Mkuu Wa wilaya hiyo kupokea mtambo Wa kutengenezea barabara aina ya loader
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiongea na waandishi Wa habari Mara baada ya mtambo huo kufika alisema kuwa huu ni utekelezaji   wa ahadi ya utatuzi wa kero sugu ya barabara ambazo zimeharibika vibaya na kushindwa kupitika katika wilaya hiyo.
 Alibainisha kuwa kutoka na kero hiyo ambayo iiiliokuwa ikiwakabili wananchi Wa wilaya take aliamua  kutafuta mitambo imara ya ukarabati na matengenezo ya barabara zote za wilaya hiyo ili wananchi wasiendelee kuteseka tena na tatizo hilo.
“Mimi Kazi Yangu nikusikiliza kero za wananchi na kuzitolea ufumbuzi ,nilisikiliza kero sugu ya ubovu Wa barabara inayowakabili wananchi Wa Arumeru na tumeipatia ufumbuzi ,na ufumbuzi wenyewe ni kama huu Wa kuleta kifaa hichi ambacho tutakitumia pamoja na mile kijiko chetu kwa ajili ya kutengeneza barabara zote za wilaya ya Arumeru” alisema Muro
Aisha alifafanua kuwa zoezi rasmi laukarabati Wa barabara hizi utaanza jumatatu  agast 19 ambapo Barabara zote za Kata na vijiji vyote vilivyopo katika halmashauri ya Meru pamoja na Arusha Dc zitakarabatiwa.
Muro amebainisha kuwa mtambo huu Wa  barabara aina ya loader umepatikana kutokana na  juhudi zinazofanywa  na yeye kwa kushirikiana  na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe, Dkt. John Danielson Pallangyo wakiwa na nia pamoja kutatua kero zote za wananchi.
Akiongea na waandishi Wa habari mmoja wawananchi alieshuhudia upokezi Wa vifaa hivyo Loserian Akwi alisema akuwa amefurahi kuona vifaa hivyo kwani anaamini kabisa tatizo LA barabara lililokuwa likiwasumbua kwa muda mrefu limeisha
“Kwakweli tumefurahi na tunashukuru sana barabara zetu zilikuwa mbivu mno yaani haswa haswa katika kipindi cha mvua lakini naamini izi machine zitatuondolea tatizo hili natutaweza kupitisha bidhaa zetu bila usumbufu ,tunashukuru sana mkuu wetu wa wilaya kwa kutatua kero zetu pamoja na serikali yetu na Rais wetu kwajinsi anavyofanya Kazi kwa kasi ya ajabu” alisema agness kitomary
Picha ikionyesha mkuu Wa wilaya ya Arumeru akipokea  mtambo wa kutengenezea barabara aina ya loader ukiwa unashushwa nje ya ofisi halmashauri ya Meru.