Home Uncategorized AJALI YA BASI NA FUSO YAUA WATU TANO MOROGORO

AJALI YA BASI NA FUSO YAUA WATU TANO MOROGORO

0

Baadhi ya majeruhi waliopata  ajali katika eneo la nanenane manispaa ya Morogoro iliyohusisha basi la abiria na fuso aina ya Tata mali ya kiwanda cha tumbaku ( ALLIANCE) wakiwa katika hospitali ya Rufaa ya Morogoro.

…………………………………..

 FARIDA, SAID MORGORO

Siku chache baada ya ajali ya lori la mafuta kulipuka na kuungua moto mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 80, leo Agosti Watu 5 wamefaliki dunia na wengine 26,  wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyohusha basi la abiria la SAFARI NJEMA na fuso aina ya Tata mali ya kiwanda cha tumbaku cha Alliance kugongana uso kwa uso katika eneo la Nanenane Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo imehusisha basi la abiria lenye namba za usajili T212 DNU ,ambapo wamesema ajali hiyo imetokea saa  saba usiku,huku wakiishauri serikali kisitisha safari za usiku kwa mabasi aya abiria.

Kwa upande wake  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo,huku akisema  Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Nae Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa Morogoro Bi. Ritha Riyamuya, amethibitisha vifo vya watu 5 pamoja na kupokea majeruhi 26 na mmoja kati yao amesharuhusiwa.

Hata hivyo kati ya majeruhi wa ajali hiyo akiwemo Bi.Rehema wamesema kuwa walikuwa wanaenda hospitali ya Rufaaa ya Mkoa wa Morogoro kwaajiri ya kuchukua mwili wa ndugu yao ambaye alifariki katika ajali ya moto iliyotokea agosti 10 mwaka huu maeneo ya msavu manspaa ya Morogoro.