Home Uncategorized SPIKA NDUGAI AONGOZA KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO, KAMATI YA SIASA ZIARA...

SPIKA NDUGAI AONGOZA KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO, KAMATI YA SIASA ZIARA YA KIKAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MANYONI

0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa wakati alipowasili katika Ofisi ya Wilayani hiyo katika ziara ya kikazi ya siku moja Manyoni Mkoani Singida. Kushoto ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi (wa pili kushoto)

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akisalimiana na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakati alipowasili kwa ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa na kushoto ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kamati ya Fedha na Mipango na kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa kabla ya ziara ya kikazi ya siku moja Manyoni Mkoani Singida. Kulia kwake ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Msimamizi wa Mradi wa korosho Wilaya ya Manyoni, Ndg. Paul Lenjima wakati alipotembelea Shamba lililopo katika kijiji cha Mkwese Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai alioongoza kamati ya Fedha na Mipango na Kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu, Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi (kulia kwake) na Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka (mwenye kofia ya CCM)

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye kofia) akiangalia Shamba lililopo katika kijiji cha Masigati Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai alioongoza kamati ya Fedha na Mipango na Kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiangalia mkorosho uliopandwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Rehema Nchimbi tarehe 18 Januari, 2018 wakati alipotembela Shamba la korosho lilipo katika kijiji cha Masigati Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai alioongoza kamati ya Fedha na Mipango na Kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tukio lililofanyika leo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Bwana Nyuki, Ndg. Ramia Konyo wakati alipotembelea kiwanda cha asali kilichopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai yuko Wilayani Manyoni kwa ziara ya kikazi ya siku moja

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akipokea zawadi ya asali kutoka kwa Bwana Nyuki, Ndg. Ramia Konyo (kushoto) wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Kulia ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)