Home Mchanganyiko WAZIRI KABUDI AKABIDHIWA UENYEKITI WA MAWAZIRI WA SADC

WAZIRI KABUDI AKABIDHIWA UENYEKITI WA MAWAZIRI WA SADC

0
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah (kulia) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi kijiti cha uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Tanzania inapokea kwa moyo mkunjufu , tena kwa heshima kubwa.Tanznaia imepokea kwa heshima kubwa uenyekiti wa kamati ya Baraza la Mawaaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, ameishukuru Jamhuri ya Watu wa Namibia kwa kusimamia vyema nafasi hii kwa mwaka mzima uliopita,” alisema Profesa Kabudi.

Profesa Kabudi anapokea nafasi hiyo kutoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri linalojumuisha mawaziri wa nchi za Nje kutoka nchi wanachama wa Sadc, utakaodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uenyekiti wa Tanzania katika jumuiya hiyo.

Akizungumza wakati wa kupokea wadhifa huo leo, Profesa Kabudi amesema anaona fahari kwa kuwa nafasi ya Tanzania katika Sadc ni ya kipekee kutokana na ushiruki wake katika kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.

Profesa Kabudi amesema nafasi hiyo ya uenyekiti wa mawaziri katika mkutano huu wa 39 wa SADC unakumbusha jukumu zito ambalo Tanzania ililibeba katika Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.

Awali, mwenyekiti wa Baraza hilo alikuwa Naibu Waziri Mkuu wa Namibia anayeshughulikia Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa, Netumbo Ndaitwah, ambye nchi yake ndiyo iliyokuwa mwenyekiti wa mkutano wa 38 wa SADC, ambayo inamaliza muda wake rasmi wiki hii.

Amesema kumbukumbu hiyo inabebwa katika maeneo ya Kongwa, Nachingwea, Mgagao na Mazimbu ambayo yaliwahifadhi wapigania uhuru wa Msumbiji, Namibia, Botswana, Angola na Afrika Kusini ambao walipata hifadhi na mafunzo kwa ajili ya kwenda kuzikomboa nchi zao.

Amesema wakati akipokea uenyekiti huu, nchi wanachama wanahitaji kuelekeza nguvu katika mapinduzi ya viwanda kwa ajili ya kuzalisha ajira na uzalishaji mali, suala ambalo ndilo kipaumbele chao kwa sasa.

“Hakika, Umoja wetu katika SADC ndiyo nguvu yetu. Wakati huu tunapofanya mkutano huu wa 39 tunakumbuka pia miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere, ambaye alichangia kiasi kikubwa katika kuanzishwa kwa umoja huu,” amesema.

Profesa Kabudi  amesema hakuna nchi inayoweza kujitegemea yenyewe katika kufikia adhma hiyo kwa sasa, hivyo ushirikiano huu utasaidia katika kuweka na kusimamia sera wezeshi kwenye uwekezaji na ujenzi wa viwanda katika nchi za SADC kwani  zinahitajika sera wezeshi na kuondoa vikwazo vya kibiashara katika maeneo yote ya nchi wanachama.

Awali, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, Ndaitwah alieleza kusikitishwa kwao na ajali ya mlipuko wa lori la mafuta mkoani Morogoro na kusababisha zaidi ya vifo 75, kisha kutoa pole kwa Serikali ya Tanzania.

Alisema uwepo wake Tanzania kwa sasa anakumbuka  miaka ya 1980 alipokuwa aakiishi nchini akijulikana kama ‘Mama Swapo’ ambapo aliiona Dar es salaam kama nyumbani kwake.

Ameshukuru kwa hatua iyofikiwa katika kutekeleza malengo ya mkutano wa 30 ambao ulilenga zaidi kuangalia miundombinu na uwezeshaji wa vijana, ambapo wameweka mikakati mizuri ya kuwawezesha vijana katika ujasiriamali.

“Ninapenda kuzipongeza Serikali na wanachi katika nchi hizo kutokana na kufuata misingi ya demokrasia na kumaliza chaguzi kwa amani,” alisema.

“Tunashukuru pia kwamba nchi sita ambazo ni ESwatini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jamhuri ya Madagascar, Muungano wa Comoros, Jamhuri ya Malawi na Jamhuri ya Afrika Kusini kwakuwa zimefanya uchaguzi huru na wa haki wa kidemokrasia na kumaliza salama kwa amani.

Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akitoa hotuba yake mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika Dr. Stergomena L. Tax akizungumza katika mkutano huo wa baraza la Mawaziri wa SADC.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu waliokufa kwa ajali ya moto na watu wengeni kujeruhiwa mkoani Morogoro.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja.