Home Mchanganyiko RC MAKONDA AJA NA MPANGO WA KUWAJIBISHA WANAUME WANAOJERUHI MIOYO NA HISIA...

RC MAKONDA AJA NA MPANGO WA KUWAJIBISHA WANAUME WANAOJERUHI MIOYO NA HISIA ZA MABINTI

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametangaza mpango wa kuanza kuwachukulia hatua Kali za kisheria wanaume wenye tabia za kudanganya kinadada kuwa watawaoa na baada ya kupata kile wanachokitaka wanaingia mitini.

RC Makonda amesema mpango huo utaenda sambamba na kusajili ndoa zote zilizofungwa Kidini Ikiwemo za Kikristo na Kislamu pamoja na zile za Kiserikali ili kinadada wawe na uwezo wa kupata taarifa za kutambua kama mwanaume ameoa na ana familia ya watoto wangapi jambo litakalosaidia kupunguza Magonjwa ya Zinaa, kulinda ndoa na pia kupunguza maumivu kwa kinadada wanaodanganywa kila kukicha.

Hatua hiyo ya RC Makonda imekuja baada ya kupokea malalamiko ya kinadada wengi waliojeruhiwa mioyo na wanaume waliowaamini na kujitolea maisha yao wakiamini wataolewa na mwisho wa siku wameishia kuachwa na kupotezewa muda jambo lililopelekea baadhi yao kutamani kujiua huku wengine wakijikuta wanapoteza ufanisi kazini.

Aidha RC Makonda amesema katika Mkutano wa Viongozi wakuu wa SADC watapata uzoefu kwa mataifa mengine kujua sheria inazungumza nini kwa wanaume wanaotoa ahadi kwa kinadada kuwa wataoa na mwisho wa siku kuingia mitini.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema kuwa baada ya kumalizika kwa Mkutano wa SADC ataitisha Mkutano na Kinadada wote waliodanganywa na kupotezewa muda ili wanaume waliosababisha hilo waanze kuwajibishwa.

Mpango huo wa RC Makonda haulengi kuwanufaisha wanawake waliodanganywa na wanaume bali pia utawajibisha wanawake waliowadanganya wanaume.

Kumbuka: KUTOA AHADI BILA KUTIMIZA NI KOSA KISHERIA.