Home Mchanganyiko WADAU NGOs WAANZA ZOEZI LA USAJILI  KATIKA KANDA YA NYANDA ZA JUU...

WADAU NGOs WAANZA ZOEZI LA USAJILI  KATIKA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI  

0
Na Mwandishi Wetu Mbeya
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maybe ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wat’s inaendelea na zoezi usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa Kanda ya Nyanda za Juu  Kusini ili kuhakikisha kuwa asasi zote zinazofanya shughuli za kijamii na kiuchumi katika ngazi za jamii zinajisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa mabadiliko ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 3 ya mwaka 2019.
Hayo yamesemwa leo jijini Mbeya na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw Erasto Ching’oro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la usajili wa NGOs zilizo nje ya Sheria.
Bw. Erasto Ching’oro amesema kuwa mapema leo kuwa Wizara iko katika hatua ya mwisho ya kukamilisha usajili wa NGOs zilizosajiliwa awali chini ya Sheria nyingine ambazo zinatakiwa kukamilisha usajili wao chini ya Sheria ya NGOs kabla ya tarehe 31 Agosti, 2019. 
Ameongeza kuwa usajili katika Kanda ya Nyanda za juu kusini utafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 13- 17 Agosti, 2019 na utajumuisha wadau wa NGOs kutoka mikoa ya Rukwa, Ruvuma, Iringa, Njombe, Katavi, Songwe na Mbeya pamoja na maeneo mengine na unafanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa jijini Mbeya.   
Bw. Ching’oro ametoa wito kwa wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutumia kikamilifu muda uliotolewa kusajili NGOs zao ili kukamilisha zoezi la kuhamisha usajili katika muda elekezi wa miezi miwili ambao ulianza tarehe 1 Julai, 2019 na utahitimishwa tarehe 31 Agosti, 2019.
“Mabadiliko ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 3 ya mwaka 2019 inayataka Mashirika yote yaliojisajili chini ya Sheria nyinginezo kuhakikisha yanakamilisha uhamisho wao ndani ya kipindi cha miezi miwili kuanzia siku ya tarehe 1 Julai, 2019 hadi 31 Agosti, 2019 ili kuendelea kuwa na haki na hadhi ya kuendesha shughuli zao katika jamii kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.  Alisisitiza Bw.Ching’oro. 
 Ameongeza kuwa zoezi la kuhuisha usajili wa mashirika yanayofanya kazi za kijamii na kiuchumi katika ngazi ya jamii lina umuhimu ukubwa maana litawezesha kuwa na matumizi bora ya rasilimali za nchi kwa kuwa na mgawanyo wenye uwiano wa afua mbalimbali za huduma za kijamii, wananachi watahamaishwa kuchangia maendeleo yao, kukuza ajira na kuongeza maarifa katika uendeshaji wa miradi ya kijamii na kukuza uwazi na uwajibikaji kwenye miradi shirikishi jamii.   
Usajili huu ulizinduliwa Kitaifa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb.) katika Kanda ya Mashariki jijini Dar es salaam mapema tarehe 10 Julai, 2019 na unahitimishwa katika Kanda ya Nyanda za Juu kusini mkoani Mbeya siku ya tarehe 17 Agosti, 2019 jijini  Mbeya.