Home Mchanganyiko TANZANIA YASHAURIWA NA WAKENYA KUAMKA KATIKA SOKO LA PARACHICHI

TANZANIA YASHAURIWA NA WAKENYA KUAMKA KATIKA SOKO LA PARACHICHI

0

************

NJOMBE

Kilimo cha parachichi kimeendelea kukua Tanzania hususani katika mikoa ya nyanda za juu kusini ukiwemo Njombe, Mbeya na Iringa na kuchangia pato kubwa la taifa licha ya changamoto ya soko la moja kwa moja kuendelea kuwa tatizo.

Kutokana na changamoto hiyo wataalamu wa kilimo kutoka nchini Kenya wamesema njia pekee ya kukabiliana na tatizo la nchi yao kugonga nembo ya Kenya katika mazao yanayozalishwa Tanzania ni wakulima kuunda vyama vikubwa na vyenye nguvu vitakavyokuwa na uwezo wa kwenda nchi za ulaya ambako masoko yaliko kutafuta mitandao ya masoko itakayowasaidia kulifikia soko bila kupitia Kenya.

Ushauri huo umetolewa mkoani Njombe na mtaalamu wa kilimo kutoka nchini Kenya Joseph Musuya alipokutana na wakulima wa parachichi kujadili mstakabali wa soko la malighafi hiyo ambayo uhitaji wake soko umeendelea kukua kila uchwao ambapo amesema wakenya wanapata faida kubwa kupitia mazao ya Tanzania kwani wamekuwa wakinunua kwa bei nahafuu na kuyauza kama zao la Kenya bei ya juu hatua ambayo inakuza pato la wanunuzi na taifa kwa ujumla.

Awali akitoa ushauri kwa wakulima Frank Msigwa ambaye ni mwenyekiti wa mtandao wa wakulima wa parachichi mkoani Njombe NISHIDA amesema wakulima wanapaswa kuachana na kilimo cha mazoea na badala yake wafanye kilimo biashara ili kuwa na uhakika wa soko la kimataifa badala ya kutegemea wanunuzi wa Kenya.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima akiwemo Editha Kayoka Prosper Kawili na Emmanuel Msigwa wanakiri kwamba elimu waliyoipata kutoka kwa mtaalamu huyo wa Kenya umehimarisha uelewa wao na kuahidia kwenda kufanyika kazi katika kilimo hicho

Katika hatua nyingine wakulima hao wameomba usaidizi wa kitaalamu katika kumaliza changamoto ya magonjwa ya fangasi, masoko,viwanda vya kuchakata mazao hayo ili kuongeza tija zaidi katika uzalishaji.

Zaidi ya tani elfu tatu za parachichi huzalishwa kila mwaka mkoani Njombe na kuingiza mabilioni ya fedha za kigeni.