Home Mchanganyiko Siwezi kuwa na amani moyoni huku mnalia

Siwezi kuwa na amani moyoni huku mnalia

0

Waziri Biteko wa tatu kulia mstari wa mbele akiangalia mchanga wenye
madini ya Chuma katika eneo la Michiga wilayani Nanyumbu.

Mzee Faya Bozani Mussa akitoa kero kwa waziri wa madini Doto Biteko
alie kaa pembeni kumsikiliza kuhusu kilio chao cha eneo la kuchimba
madini ya Chuma Michiga.

Mkuu wa Wilaya Nanyumbu Moses Machali akiongea na wananchi wa
Kata ya Nanyumbu kabla hajamkaribisha wazi wa Madini Doto Biteko
kushoto kwake ili azungumze na wananchi.

Waziri Biteko wa tatu kulia na wa kwanza kushoto Mkuu wa Wilaya
Nanyumbu Moses Machali wakimsikiliza Arafati Omar Mrope mwekezaji wa
madini ya Chuma Michiga wengine.

****************

Na Issa Mtuwa “WM” Nanyumbu Mtwara

Sikuzote katika sehemu ya maisha yangu nikiwa kama Waziri wa Madini,
hakuna kitu kinachonisononesha na kunikosesha amani moyoni kama
ninapofika mahali au kuona kwenye vyombo vya habari wananchi tena
wanyonge wanalia na kunyanyasika kisa wanakosa maeneo ya kuchimba,
wanalilia leseni ama mwekezaji wana wanyanyasa wakati rasilimali hizo
zinawazunguka kwenye maeneo yao.

Haya yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko tarehe 12/08/2019
wakati akiongea na wananchi wa kata ya Michiga wilaya ya Nanyumbu
mkoani Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kufuatia ziara
yake wilayani humo kukagua shuguli mbalimbali za sekta ya madini na
kutatua wananchi wanamlilia na kumpigia magoti kuomba eneo baba
chondechonde tunaomba tusaidie eneo lile tuchimbe.

Katika ziara yake katika mikoa ya Lindi na Mtwara Biteko amekutana na
kilio cha wananchi karibu kila mahali kukosa maeneo ya kuchimba madini
huku raslimali hizo zikiwa zimewazunguka.

“Mhe. Waziri kuja kwako leo tunakushukuru sana, Babaa kiliochetu sisi ni
eneo la kuchimba baba tafadhali chondee tunaomba turuhusu tukachimbe,
tupate riziki babaaaa, pale palipo fungiwa hata sisi tunaathirika kwa sababu
palikuwa panatusaidia” alisema Mzee Faya Bozani Mussa alipopata fursa
ya kuongea mbele ya waziri Biteko.

Kufuatia kilio hicho akiwaangalia kwa huruma na kwa kuonyesha kuguswa
na wananchi hao waziri Biteko papo hapo hakutaka kuwa chukuwa muda
kutatua kero hiyo alitoa kauli na iliyo geuza huzuni kuwa furaha ya
wananchi walio kusanyika kwa wingi katani hapo.

“Ndugu zangu, poleni sana, naumia sana moyoni kuwaona mnasononeka
moyoni kwa ajili ya raslimali zinazo wazunguka. Rais wetu Dkt. John
Pombe Magufuli anawapenda sana na mimi ameniteuwa kumsaidia lakini
kazi yangu aliyo nituma ni kuja kutatua kero za wananchi katika sekta ya
madini na ndio maana nipo hapa Michiga siku ya leo.”

“Mimi ni mtumishi wenu, nipo hapa kuwatumikia sipo teyari kuondoka hapa
huku bado machozi yakiwa yanaendelea kutiririka. Sasa nisikilizeni. Moja,
naagiza Tume ya Madini ifikapo ijumaa ijayo tarehe 16/08/2019 leseni ya
lile eneo iwe imeshafika kwa Mkuu wa Wilaya ili yeye na afisa Madini Mkazi

Mkoa wa Mtwara waje wakabidhi hiyo leseni. Pili, safari yangu
nimeambatana na Mkurugenzi Ukaguzi Migodi na Mazingira kutoka Tume
ya Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga yule pale, yeye atabaki hapa
hataondoka japo kesho ilibidi aondoke kwa ajili ya majukumu mengine
lakini hataondoka ili yule mwekezaji wenu Arafati Mrope amsaidie kuandaa
mpango kazi wa lile eneo ili ikifika leseni kazi ianze. Dkt. Utabaki hapaa”
alisema Biteko.

Maelezo hayo yaliibua shangwe, vigelegele, nderemo na vifijo kwa
Wanamichiga na kusahau kilio chao.

Kufuatia kauli hiyoo Mwenye (Chief) Njawala alisimama na kuishukuru
serikali na kuipongeza huku akisema kauli ya waziri imeondoa minong’ono
iliyokuwa imetanda ikiwatuhumu viongozi wa ngazi mbalimbali kuwa ndio
waliokuwa wanawazuia wasichimbe wakati taratibu za kuchimba zilikuwa
hazijazingatiwa.

“Mhe. Waziri Mimi ni Chief wa eneo hili, nakushukuru kwa kutatua tatizo hili
na umeleta amani maana awali viongi mbalimbali ndio walio kuwa
wanatuhumiwa kwamba ndio wanaozuia, binafsi nakushukuru sana”
alisema Chief Njalawa.

Eneo Michiga limezungukwa na madini ya Chuma eneo ambalo lilikuwa
limechukuliwa na mwekezaji Arafati Omari Mrope aliekuwa anachimba na
kununua madini hayo kutoka kwa wananchi na baadae eneo hilo kuzuiwa
na serikali kwa kuwa waliokuwa wanafanya shuguli hizo walikuwa
wanafanya kinyume cha sheria.

Kwa upande mwingine Waziri Biteko alimshukuru na kumpongeza
mwekezaji Arafati kwa kwa utii kwa serikali kwani hata alipo simamishwa
asiendelee na kazi ya uchimbaji wa madini hayo mpaka afuate utaratibu
kwa maana apate leseni alikubali na hakuendelea huku akilipa madeni ya
zaidi ya Tsh. 35,000,000/= kwa wananchi waliokuwa wanachimba
mchanga wa madini ya Chuma na kumuuzia mwekezaji huyooo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali alimshukuru Waziri
wa Madini Doto Biteko kwa kufanya ziara hiyo na kutatua kero hiyo papo
hapo bila kusubiri.

“Mhe. Waziri nakushukuru sana kwa ujio wako, na maamuzi ya papo kwa
papo na hiyo ndio speed ya serikali ya awamu ya tano katika kutaatua kero

za wananchi hasa katika kufanyaa maamuzi yanayogusa maisha ya
wananchi wetu moja kwa moja” alise Machali.

Kabla ya mkutano huo Biteko alikutana na kufanya kikao cha ndani na
viongozi wa Wilaya ya Nanyumbu wakiongozwa na mkuu wa wilaya Moses
Machali ambapo alisomewa taarifa ya wilaya kuhusu hali ya sekta ya
madini.