Home Mchanganyiko SERIKALI KUJENGA MNALA MAKABURI YA WALIFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO MOROGORO

SERIKALI KUJENGA MNALA MAKABURI YA WALIFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO MOROGORO

0

**************

STORY NA FARIDA SAIDY, MOROGORO

Serikali imesema itajenga mnala katika makaburi ya watu waliofariki
katika ajali ya moto ilitokea agosti 10 mwaka huu eneo ya msavu na
kusababisha vifo watu 75 na majeruhi 59,ambao wanaopatiwa
matibabu katika hospitari ya taifa muhimbuli na hospitari ya rufaa ya
Morogoro.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh Kassimu Majaliwa agosti 12 katika makaburi ya kola hill
manspaa ya Morogoro,ambapo amesema kuwa ni ruksa kwa familia
kufanya maombi katika makaburi hayo.

Imeutaka uongozi wa mkoa wa Mrogoro kujenga mnala utakaoyafanya
makaburi hayo kutambulika na kuwa kama sehemu ya kumbukumbu
kwa ndugu wa marehemu.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewashuru viongozi mbalimbali
wa kiserikali,Dini na siasa walijitokeza kwa namna moja na nyingine
pamoja na madaktari wanaowasaidia wajeruhi kuapata matibabu.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ametoa pole
watanzania wote hususani Wanamorogoro ambapo walioshiriki katika
msiba huo na kuwataka kuimarisha umoja wao kama ilivyodesturi ya
watanzania.

Aidha Mh Mhagama amewataka watanzania ambao wanasiwasi kuwa
ndugu zao wamepoteza maisha katika ajali hiyo kujitokeza kwa ajili ya
kupima vinasaba na kutambua miili ya ndugu zao.

Katika upande wa majeruhi Dk Kebwe amesema kuwa mpaka sasa
majeruhi wote wanaendelea vizuri huku 16 waliopo katika hospitari ya
Mkoa wa Morogoro wameanza mazoezi ya kutembea.