Home Mchanganyiko Prof.Kabudi amekagua pikipiki zitakazotumika kuongoza misafara ya viongozi SADC

Prof.Kabudi amekagua pikipiki zitakazotumika kuongoza misafara ya viongozi SADC

0

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa anafurahia mojawapo ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam,Tanzania. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji – IKULU Bw. Zuberi Kachingwa.

Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi nakala za hati za utambulisho. Tukio hilo limefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya pikipiki mpya zitakazotumika katika mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam zikiwa tayari kwa mapokezi.

Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet akiwatambulisha kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi baadhi ya maafisa aliongozana nao,wakati alipofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhi nakala za hati za utambulisho.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet pamoja na Wakurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw Jestas Nyamanga na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.