Home Mchanganyiko IKUPA:ANAYEPINGANA NA MAGUFULI ANAPINGANA NA MUNGU MWENYEWE

IKUPA:ANAYEPINGANA NA MAGUFULI ANAPINGANA NA MUNGU MWENYEWE

0

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa akiwasili katika ukumbi wa CCM Mkoa Dodoma kwa ajili ya kufunga  Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa akisalimiana na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UWT,Bi.Chiku Mugo alipowasili katika ukumbi wa CCM Mkoa Dodoma kwa ajili ya kufunga Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa akisalimiana na Mbunge wa viti maalum Mariam Ditopile alipowasili katika ukumbi wa CCM Mkoa Dodoma kwa ajili ya kufunga Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa,akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Jesca Mbogo wakati wa  kufunga Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wakifatilia kikao cha baraza Kuu la UWT mkoa wa Dodoma

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa,akiwa pamoja na wajumbe wakipitia taarifa wakati wa kufunga Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma.

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa,akizungumza na wajumbe  wakati wa  kufunga Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma upande wa kushoto ni Mwenyekiti wa UWT mkoa Neema Majule.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

……………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa amesema watu wanaombeza na kupinga jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Dkt.John Magufuli watakuwa wanapingana na Mungu Mwenyewe.

Mhe.Ikupa amesema hayo  jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT]Kwa mkoa wa Dodoma.

Mhe.Ikupa amesema mambo Mengi yaliyokuwa kwenye ilani ya Uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa Chama Cha Mapinduzi yametekelezwa na kubainisha kuwa mtu ambaye hajaguswa na jitihada za Rais Magufuli atakuwa Muongo.

Aidha,Ikupa ametaja Nyanja ambazo Serikali ya awamu ya Tano imetekeleza ikiwa ni pamoja na kupambana na Dawa za kulevya ambazo zilikuwa zikipoteza vijana na kurudisha nyuma uchumi wa nchi,Uimarishaji wa Miundombinu ni pamoja na Umeme,Barabara,Reli na Usafiri wa anga pamoja na uwezeshaji wa Mikopo kwa makundi maalum ikiwa ni pamoja na vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.

Hata hivyo ,Naibu Waziri huyo amechangia Jumla ya mabati 10 yenye thamani ya Tsh.360,000 Kwa UWT Dodoma kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu huku jumla ya Tsh.milioni moja ,laki nane na hamsini elfu zikichangiwa kwenye harambee ya baraza hilo.

Awali akizungumza katika kikao hicho,mwenyekiti wa UWT mkoa Neema Majule amesema tangu wanaingia madarakani waliahidi mambo matatu ikiwemo kujenga UWT yenye upendo,umoja na mshikamano na kupitia mikutano mbalimbali tuliyoifanya hilo wamefanikiwa.

“Kwa sasa tumebaini na kushughulikia upatikanaji wa viwanja vya uwekezaji,na hili tumelifanya kila wilaya nia yetu tujitegemee na tusiwe tegemezi,”alisema mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake mjumbe wa Baraza kuu Taifa UWT,Chiku Mugo amempongeza Naibu Waziri Ikupa Kwa Mchango huo huku akiwapongeza wadau wengine kwa kuendelea kuiunga UWT Katika kufanikisha miradi mbalimbali ya
Maendeleo.