Home Mchanganyiko WATOA HUDUMA FANYENI KAZI BILA KUSUKUMWA

WATOA HUDUMA FANYENI KAZI BILA KUSUKUMWA

0
Mkurugenzi Dkt.Grace Magembe wakiongea na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya iringa Dkt.Alfred Mwakalebela
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Grace Magembe akiongea na watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa (hawapo pichani),kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya hospitali hiyo Bi.Elisifu Mafole na kushoto ni mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt.Alfred Mwakalebela
Mkurugenzi wa Utawala na Rasiliamali watu Bi.Deonatha Makani akifafanua jambo wakati wa kikao cha wakurugenzi wa wizara na watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa ya iringa
Mwenyekiti wa waganga wafawidhi wa hospitali za mikoa Dkt.Ibenzi Ernest akielezea huduma za kibingwa walizotoa kwa muda wa wiki mbili kwenye hospitali hiyo
Watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa wakimsikiliza mkurugenzi wa tiba(hayupo pichani)ambapo walitakiwa kufanya kazi bila ya kusukumwa na kuonyesha mabadiliko katika utoaji wa huduma za afya
…………………
Na.Catherine Sungura,WAMJW-Iringa.
Watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma bila kusukumwa na mtu yeyote.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa idara ya tiba kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Grace Magembe wakati akiongea na watumishi wa hospitali hiyo ikiwa ni ziara ya kujionea huduma za kibingwa zilizofanywa katika hospitali hiyo ambazo zimetolewa na madaktari bingwa kutoka wizarani.
Dkt.Magembe alisema kuwa amepokea majina ya Watumishi ambao wamepewa onyo mara kadhaa na wameshindwa kubadilika hivyo watachukuliwa hatua kulingana na taratibu za kiutumishi.
” Wengine mtapewa muda wa kujirekebisha na kufuatiliwa kuona kama mmebadilika,sitegemei kufukuza mtaalam yeyote kwani wanayo nafasi ya kubadilika”.
“Kama mtumishi wa umma na ulipewa viapo hivyo mnapaswa kufanya kazi bila kusukumwa kwani kwenye utumishi wa umma hakuna kubebana”.Alisisitiza Dkt.Magembe
Aidha, alisema kuwa wananchi wanawategemea wataalam hao katika kutoa huduma za afya zinazostahili.
“Mgonjwa anapokuja hospitali ya rufaa ya mkoa anatakiwa kuona mabadiliko kuanzia lugha nzuri na huduma kwa mteja izingatiwe,lazima utofauti uwepo wa hospitali ya mkoa na vituo vya huduma vilivyopo chini”.Alisema Dkt.Magembe.
Akitoa ripoti ya huduma za kibingwa zilizofanywa na madkatari hao Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa dodoma ambaye ni mwenyekiti wa waganga wafawidhi Tanzania bara Dkt.Ibenzi Ernest alisema tangu huduma hizo kutolewa mwishoni mwa mwezi wa saba mwaka huu wamewaona wagonjwa 656,wagonjwa 41 wamefanyiwa vipimo na wagonjwa 88 wamepata huduma za upasuaji .
Dkt.Ibinza alisema huduma za kibingwa zilizotolewa ni pamoja na upasuaji,mifupa,magonjwa ya ndani na pua,koo na masikio.
Wizara ya afya imeamua kutoa huduma za kibingwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya kuboresha na kuwajengea uwezo madaktari bingwa waliopo hospitalini hapo kwa majuma mawili.