Home Mchanganyiko MAJALIWA AKAGUA UNUNUZI WA PAMBA WILAYANI ITILIMA NA MASWA NAKUZINDUA MIFUMO

MAJALIWA AKAGUA UNUNUZI WA PAMBA WILAYANI ITILIMA NA MASWA NAKUZINDUA MIFUMO

0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mwananchi baada ya kukagua ununuzu wa pampa katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Maendeleo Luguru na Itubilo wilayani Itilima, Agosti 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mfumo wa Kielektroniki wa Kusimamia Biashara (Agricultural Trade Management Information System (ATMIS) wakati alipohitimisha Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati Mkurugenzi wa Kampuni ya Nsagali, Emmanuel Gangu Silanga (kushoto) alipomkabidhi fedha Katibu Mkuu wa Chama cha Ushirka cha Msingi cha Maendeleo Luguru na Itubilo, Bibi Buzo Hussein kwa ajili ya kuwalipa walikuma watakaouza pamba kwenye chama hicho. Kampuni hiyo imeahidi kununua pamba yote mkoani Simiyu na imemhakikishia Waziri Mkuu kuwa inazo pesa za kutosha. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya kukagua ununuzi wa pamba, Agosti 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kumalija cha wilayani Maswa Agosti 8, 2019. Waziri Mkuu alikuwa katika ziara ya kukagua ununuzi wa pamba katika mkoa wa Simiyu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).