Home Mchanganyiko Waziri Ummy, Balozi Misri wakubaliana uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini

Waziri Ummy, Balozi Misri wakubaliana uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini

0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa (kushoto) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam leo.  Kulia ni ofisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, Ahmed El- Ghoul  na Ofisa kutoka wizara ya Afya.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa. Kushoto ni ofisa kutoka Wizara ya Afya na  na kulia ni ofisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, Ahmed El- Ghoul.

Captions: Picha na John Stephen

************

Na John Stephen

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa na kujadiliana kuhusu kushirikiana katika kuboresha huduma za afya nchini.

Katika mazungumzo hayo pande mbili zimependekeza kushirikiana pamoja katika  uwekezaji wa viwanda vya dawa na chanjo, kubadilishana wataalam wa afya ili kuwajengea  uzoefu wataalam wetu katika nyanja mbalimbali za sekta  nchini.

Pia, Waziri Ummy Mwalimu kwa pamoja wamekubaliana  kwa pamoja kuendeleza mapambano ya Homa ya Ini aina C  (Hepatitis C) ili kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora na kwa wakati kuhusu homa ya Ini aina C.

Baada ya majadiliano hayo Waziri Ummy Mwalimu aliagiza kuandaliwa kwa hati ya ushirikiano (MOU) kwa ajili ya kuratibu na kutekeleza  maeneo mbalimbali ya kipaumbele katika sekyta ya afya nchini.