Home Mchanganyiko Waziri Simbachawene atoa wito kutangaza mafanikio ya Muungano 

Waziri Simbachawene atoa wito kutangaza mafanikio ya Muungano 

0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao na viongozi mbalimbali na watendaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar alipofanya ziara ya kujitambulisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Simbachawene, ujumbe wake, viongozi, watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao na viongozi mbalimbali na watendaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Viongozi na watendaji wa Serikali wakifuatilia kikao kilichowakutanisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Simbachawene.
*************
Na Ofisi ya Makamu wa Rais
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Simbachawene amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kipekee na kuwataka Watanzania kutangaza mazuri yake.
Ametoa kauli hiyo Agosti 5, 2019 wakati wa ziara yake visiwani Zanzibar alipofika kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar.
Waziri Simbachawene alisema kuwa Muungano wetu unaishi na kuwa ni vyema sasa tuyape sauti kubwa yale mazuri yanayofanyika kutokana na Muungano huo kuliko changamoto.
“Mazuri ya Muungano ni mwngi kuliko changamoto na nina imani tutashirkiana vizuri na kaka yangu hapa Mheshimwa Aboud ambaye ni mwanadiplosia na tuna wataalamu hapa mtatusaidia ili tutekeleze wajibu. 
Niwahakikishie nitachangia mawazo katika kuutunza na kuulinda, naomba ushirikiano,” alisisitiza Waziri Simbachawene. 
“Changamoto zilizokuwepo 15 hadi sasa zimebaki kama tano zingine zinapungua zaidi muungamo unaishi aina ya muungano ni haufanania  na mingine ni vizuri kulinda kutunza na kuuendeleza na wakati mwingine ni vizuri kuangalia na kuona umuhimu wa kueleza mazuri yake.
“Wakati sasa umefika kwa kizazi kilichozaliwa ndani ya karne ya 21 kinapaswa kuelewa dhamira nzima ya waasisi wa Muungano ambao wengi kati yao wamesoma historia yake ndani ya vitabu,” alisisitiza.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud alisema Serikali hizi mbili zina jukumu la kuutunza na kuuendeleza Muungano.
Mhe. Aboud alisema Ofisi hizi za Makamu wa Rais na Makamu wa Pili zinahitaji kufanya kazi kwa pamoja na kuwa urafiki wetu utakuwa chachu ya kufanya kazi kwa ukaribu zaidi.
“Nakukukaribisha sana Mheshimwa Waziri na milango ipo wazi na tunaweza kushirkiana kwa karibu tufanye kazi pamoja ili tutekeleze wajibu wetu katika kusimamia mambo ya Muungano,” alisema Mhe. Aboud.