Home Mchanganyiko MSAADA WA KISHERIA WATOLEWA KWA WANANCHI KATIKA MAONYESHO YA 8 8 SIMIYU

MSAADA WA KISHERIA WATOLEWA KWA WANANCHI KATIKA MAONYESHO YA 8 8 SIMIYU

0
Wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na sheria wakiwa katika Banda la Wizara tayari kutoa huduma ya Msaada wa sheria kwa wananchi watakaotembelea Banda lao.
Wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na sheria katika picha ya pamoja tayari kuanza kutoa hudum a ya Msaada wa sheria kwa wananchi watakaotembelea Banda lao.
Wanafunzi wa Simiyu Sekondari wakisoma machapisho mbalimbali ya sheria kwenye Banda la Wizara ya Katiba na Sheria katika viwanja vya Nyakabindi yanakofanyika maonyesho ya Kitaifa ya 8 8 mkoani Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza kitu alipotembelea Banda la Wizara ya Katiba na Sheria katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu
……………………
Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ipo Kanda ya Ziwa Mashariki – Simiyu katika maonyesho ya Wakulima 8 8 Kitaifa mkoani Simiyu na kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi wanaotembelea Banda la Wizara.
Katika maonyesho hayo Wizara ya Katiba na Sheria inashirikiana na asasi zisizo za kiserikali ambao ni wadau wake kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi mbalimbali wenye uhitaji ambao wanatembelea maonyesho hayo.
Katika maonyesho hayo Wizara na wadau wake pia  wanatoa elimu ya sheria mbalimbali kama vile sheria za mirathi, ndoa, talaka, kumiliki mali na sheria ya mtoto kwa wananchi na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za mkoani Simiyu ambao wanatembelea Banda la Wizara.
Katika maonyesho hayo Wizara inawasisitiza wananchi kutumia huduma ya Msaada wa kisheria ambayo inatolewa ana Serikali kwa wananchi wenye uhitaji kuwa ni haki  yao na hivyo wajitokeze kwa wingi Ili waweze kuhudumiwa na kuelimishwa juu ya masuala mbalimbali ya kisheria nchini Ili waweze kupata haki zao pale wanapostahili.
Msaada wa kisheria ni haki ya kila mwananchi mwenye uhitaji kama ambavyo Sheria ya Msaada wa Sheria No. 1 ya mwaka 2017  inavyosema .
Mwananchi Njoo utembelee Banda la Wizara ya Katiba na Sheria update kusikilizwa na uhudumiwe kwa kupata ushauri wa kisheria bila ya kulipia huduma hiyo katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.